KUTATUA CHANGAMOTO YA UVUJAJI WA MAJI KUPITIA “CONCRETE GUTTER” KWENYE NYUMBA AINA YA “CONTEMPORARY”.
Kuzuia maji yanayovuja kwenye paa la “contemporary house” kupitia concrete gutter, ni changamoto inayohitaji umakini, ubunifu na mbinu ya ziada kutokana na kwamba maji huwa na ung’ang’anizi na ubishi mkubwa pale yanapokutana na udhaifu wa aina yoyote ile. Baada ya maji ya mvua kushukia kwenye “gata ya zege(concrete gutter)” katika maeneo yanayopita maji mara nyingi huwa na mifereji midogo inayokusanya maji hayo na kuyapeleka kwenye bomba zilizosimama wima(vertical ducts) ambazo huyashusha chini, mifereji hii pia mara nyingi huwa chanzo cha maji kuvujia kwenye kuta au sakafu.
-Kadiri sakafu inavyokuwa na mteremko mkali zaidi ndivyo kadiri inavyokuwa salama zaidi dhidi ya maji kuvuja kwani mteremko huruhusu maji kukimbia kwa kasi kabla ya kuzama kwenye zege. Pia sakafu ambayo ni rafu ina nafasi kubwa zaidi ya kuvujisha maji kuliko sakafu ambayo imefanyiwa finishing laini ya mwisho.
-Njia nyingine ya kuzuia maji kuvuja kutokea kwenye gata ya zege(concrete gutter) ni kwa kutumia vifaa vya kimiminika na kemikali kama vile (concrete filler and sealant) kuziba maeneo yanayovuja kama kutakuwa na nyufa zinazosababisha maji kupenya.
-Njia bora kabisa ya kuzuia maji kuvujia kwenye kuta kupitia gata ya zege(concrete gutter) ni kwa kutumia zulia la plastiki maarufu kama “waterproofing membrane”.
Zulia hili ni jembamba na linatandazwa eneo lote la juu la sakafu husika. Juu ya zulia hilo la plastiki maarufu kama “waterproofing membrane” yanamwaga material mithili ya zege inayojulikana kama “concrete filler and sealant” au zege yenyewe ambayo itamwagwa katika umbo la kutengeneza mteremko utakaopeleka maji kwenye matundu yanayoshusha maji chini ardhini(vertical ducts) yaliyosimama wima. Na mwisho kumalizia kwa finishing laini au kuweka vigae vyenye uso laini vya sakafuni au ukutani (floor or wall tiles).
Arch. Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
nahitaji kujua zaidi uzuiaji maji ya gata
Karibu sana.