RANGI ZA MAJI(EMULSION PAINTS) NA RANGI ZA MAFUTA(SILK PAINTS)

Kumekuwa na aina kuu mbili za rangi za nyumba ambazo tumekuwa tunapaka kwenye kuta za nyumba, ndani na nje ya nyumba katika kupendezesha uso wa ukuta katika kiwango cha juu kabisa. Aina hizi kuu mbili za rangi ni rangi za maji maarufu kama “emulsion paints” na rangi za mafuta maarufu kama “silk paints au wash and wear”.

RANGI YA MAFUTA(SILK PAINT) HUPAKWA JUU YA RANGI YA MAJI(EMULSION PAINT)

Rangi za maji kwanza hutumika kwa kuchanganywa na chokaa za aina kadhaa kama vile “gypsum powder” au “white cement” ambapo hupakwa juu ya ukuta uliopigwa plasta ili kupata uso laini na unaoendana na rangi kabla ya kuja kupaka rangi juu yake. Baada ya kupaka aina hiyo ya chokaa iliyochanganywa na rangi ya maji(emulsion paint), ndio sasa rangi ya maji yenyewe huja kupakwa juu yake kuleta muonekano unaovutia sana na wa rangi iliyokusudiwa. Baada ya rangi ya maji kupakwa labda kwa tabaka mbili ndio rangi ya mafuta ya kuta maarufu kama “silk paint au wash and wear” huja kupakwa juu yake kuleta mng’ao mkali unavutia na kuteleza na kupendeza mithili ya “gloss”.

RANGI ZA SILK HUFANYA UKUTA KUMEREMETA

Kwa watu ambao hawako tayari kutumia gharama kubwa kwenye rangi kwa sababu zozote zile huishia kupaka rangi ya maji peke yake(emulsion paint) na kuachana na rangi hizo za mafuta(silk paints or wash and wear) ambazo huleta mng’ao na zenye kuteleza kwa sababu gharama ya rangi za silk ni kubwa zaidi ya mara tano ya gharama za rangi za maji ambazo ni bei rahisi sana. Licha ya kwamba ni za gharama nafuu sana ukulinganisha na rangi za silk, lakini changamoto ya kupaka rangi ya maji peke yake ni kwanza haina mng’ao kama rangi ya silk lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba ukuta uliopakwa rangi ya maji peke yake ukichafuka hauwezi kusafishwa na kurudi katika hali yake ya mwanzo bali hufubaa na kuacha kama doa ukutani, ambapo itakuhitaji upake rangi tena upya kuurudisha katika hali yake ya mwanzo kabla ya uchafu. Wakati ukuta uliopakwa rangi ya mafuta(silk paint) hata kama umechafuka kiasi gani ukiusafisha unarudi kwenye mnga’ao na kumeremereta kama ulivyokuwa mwanzoni. Hivyo kwa sababu ya usafi na hasa maeneo yenye changamoto kama jikoni, sehemu zenye majimaji au kama nyumba inaishi watoto wadogo rangi ya mafuta(silk paint) ni muhimu sana katika kuhakikisha kuta hizi ni safi wakati wote.

RANGI ZA MAJI(EMULSION PAINTS) HUCHANGANYWA NA CHOKAA ILI KUPAKA JUU YA UKUTA ULIOPIGWA PLASTA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

10 replies
  1. Jimmy
    Jimmy says:

    Naomba kujua mchanganyo sahihi kati ya rangi A silk na solvent.
    Pia rangi za maji uchanganywa Kwa kiasi Gani Cha maji?

    Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *