KUJENGA KWENYE ENEO LENYE MWINUKO/MTEREMKO.

Watu wengi wanaomiliki viwanja kwenye maeneo yenye mwinuko au mteremko mkali hujaribu kufikiria namna zaidi ya kutumia kiwanja chake husika kwa namna sahihi zaidi kadiri ya umbo ambalo kiwanja chake kinachukua.

KUJENGA KADIRI YA MWINUKO WA KIWANJA

Maeneo yenye mwinuko ni maeneo mazuri sana katika kufanikisha ujenzi wa jengo lenye kuvutia na linaloonekana vizuri na kwamba usahihi. Watu wengi huamua kwamba watatumia eneo la chini kama ghorofa ya chini ardhini(basement floor) huku wakitumia eneo la juu kama ghorofa ya juu(ground floor).

UKALI WA MTEREMKO NDIO UTAAMUA KAMA INAFAA KUWEKA SAKAFU YA ARDHINI (BASEMENT FLOOR)

Kitu kitakachoamua kama eneo hilo liwe na hiyo basement floor ni ukali wa mteremko husika, ambapo kama eneo mteremko wake ni wa kawaida na sio mkali sana(gentle slope), basi eneo hilo bado halitoshi kuweka (basement floor) chini kwani itasababisha kushindwa kuwa na urefu sahihi kwenda juu au kulazimisha sana kiasi cha kuharibu jengo lenyewe.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *