MISINGI YA FALSAFA YA UJENZI YA “LEAN CONSTRUCTION”

-Maboresho endelevu: Makampuni yanayotumia mfumo huu wa falsafa ya ujenzi ya “lean construction” yamewekeza sana katika kuendelea kuboresha kila siku na kutafuta namna na mbinu za kuboresha huduma za ujenzi.

FALSAFA YA UJENZI YA “LEAN CONSTRUCTION” INAHUSISHA MABORESHO ENDELEVU

-Kuepuka mabaki na uchafu: Makampuni yanayotumia falsafa hii ya ujenzi ya “lean construction” yanajitahidi kufanya kazi kupunguza mabaki ya malighafi ya vifaa na ujenzi na uchafu kuhakikisha malighafi nyingi hazihusishi utengenezaji mkubwa katika eneo la ujenzi bali nyingi zinafanyikia kiwandani, pia muda mwingi hautumiki katika kufanya kazi kwani nyingi zinakuwa zimeshafanyika nje ya eneo la ujenzi ambapo jengo lenyewe linaposimama. Hii inajumuisha kuhakikisha kwamba kazi inafanyika kwa usahihi maramoja bila kuhitaji kurudia rudia, kazi inapangiliwa kwa usahihi mwanzoni ili kuepuka kupoteza muda wakati ujenzi unaendelea kwa vitu ambavyo vilikuwa havijapangiliwa.

UCHAFU NA MABAKI YA MALIGHAFI ZA VIFAA VYA UJENZI YANAPUNGUZWA KWA KIASI KIKUBWA SANA KUEPUKA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA MALIGHAFI

-Kumridhisha mteja: Katika falsafa ya ujenzi ya “lean construction”, maamuzi yote yanayofanyika katika kubadili au kuboresha chochote kinachoonekana kinahitaji mabadiliko, lazima kihusiane na malengo na vipaumbele vya mteja.

MALENGO NA VIPAUMBELE VYA MTEJA HUZINGATIWA MARA ZOTE

-Kuheshimu wafanyakazi: Makampuni yanayotumia falsafa hii ya ujenzi ya “lean construction” yanatambua kwamba wafanyakazi wanaweza kufanya vizuri sana kama watahimizwa kuwa na ushirikiano, kuonyeshwa kuheshimiwa na kuheshimu mawazo yao na kupewa uhuru wa kutosha kutatua changamoto na kujiongeza kwa usahihi katika majukumu husika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *