NAMNA YA KUINGIZA FALSAFA YA UJENZI YA “LEAN CONSTRUCTION” KWENYE UTEKELEZAJI.

“Lean Construction” ni falsafa na sio mchakato wa hatua kwa hatua, kwa hiyo ili kunufaika na mfumo huu wa “lean construction” ni kuingiza falsafa hii katika utekelezaji katika kila kitengo cha kampuni na katika kila hatua ya ujenzi.

Mambo Ya Kufanya Katika Kutekeleza Falsafa Hii Ya “Lean Construction”.

-Kuwapa wafanyakazi uhuru zaidi wa kimaamuzi: Kila mfanyakazi anaelewa kazi yake vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kupewa nafasi na kuwahimiza kutatua changamoto wenyewe, kufanya kazi kwa ushirikiano na kutoa mapendekezo zaidi ya kuboresha. Kwa kufanya hivi unawajengea uwezo mkubwa zaidi wa kujisimamia na kuongoza wengine.

UHURU WA KIMAAMUZI UNAONGEZA SANA UBUNIFU KWA WAFANYAKAZI

-Kuzuia uharibifu wa vifaa na majengo: Vifaa huwa vinahitaji ukarabati wa mara kwa mara ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi wa viwango vya juu na hata jengo huhitaji ukarabati ili liweze kuwa katika ubora sahihi kibiashara, sasa njia nzuri ya kufanya ukarabati ni kuzuia uharibifu ambao unaweza kuzuilika badala ya kutegemea kuja kufanya ukarabati mkubwa. Kwa njia hii gharama za ukaratabati zitakuwa chini na ufanisi utakuwa juu sana.

-Kupangilia kazi mapema: Ili kuepuka kupoteza muda na wakandarasi wanapaswa kupangilia vizuri kazi yote na hata kazi inayofuata ili kusiwepo kuchelewa au kuingiliana kwa mambo kunakochelewesha kazi na kusababisha hasara za aina mbalimbali.

VIPAUMBELE VYA MTEJA NI KITU CHA KWANZA NA MUHIMU KATIKA FALSAFA HII YA UJENZI YA “LEAN CONSTRUCTION”

-Kuweka malengo yanayoendana na vipaumbele vya mteja: Katika falsafa hii ya ujenzi ya “lean Construction” maamuzi yote yanatakiwa kufanyika kwa msingi wa kuongeza thamani kwa mteja. Kama kutakuwa na hatua yoyote isiyolenga kuongeza thamani itapaswa kuondolewa. Timu zote zinahusika na ujenzi zinapaswa kukutana mwanzoni na kuweka malengo yanayoendana na malengo ya mteja.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *