NYUMBA ZA KISASA ZINAHITAJI MAANDALIZI NA MWONGOZO WA KITAALAMU KATIKA UJENZI

Ili mtu aweze kuipenda nyumba yake na kufurahia kila anapoitazama inapaswa kuwa ni nyumba nzuri inayomvutia angalau yeye binafsi. Na hii ndio sababu watu wengi wamekuwa wakivutiwa sana na aina mbalimbali za nyumba za kisasa za wakati huu ambazo zimekuwa na mwonekano na mvuto wa kipekee kutokana na mapinduzi makubwa ya kisanifu yanayoendelea sambamba na ukuaji mkubwa wa teknolojia vilivyowezesha ubunifu huu unaovutia sana tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani kidogo.

MAPINDUZI YA KISANIFU NA TEKNOLOJIA YAMEBORESHA SANA MUONEKANO WA NYUMBA ZA KISASA
LAKINI UJENZI WAKE UMEENDELEA KUWA CHANGAMOTO KWA MAFUNDI

Lakini licha ya nyumba hizi za kisasa kuwa nzuri na zenye mvuto sana bado haziwezi kumvutia mmiliki wake kama miongozi yote ya kitaalamu iliyolengwa kwenye nyumba husika haitazingatiwa. Nyumba hizi za kisasa zimekuwa na vipengele vingi vya kisanifu ambavyo vingine vinahusisha mpangilio na vingine vinahusisha ubunifu mwingine ambavyo ndivyo vinajumuisha kuleta muonekano bora na wenye kuvutia. Vipengele hivi mara nyingi kwenye ujenzi huweza kupuuzwa kama hakuna usimamizi makini unaohusisha uwepo au kutembelewa na mshauri wa kitaalamu na hivyo ule ukisasa wenyewe wa nyumba husika kupotea au kudorora sana.

MIONGOZO YA KITAALAMU NI MUHIMU KWENYE NYUMBA ZA KISASA KULIKO HATA ZILE ZA ZAMANI

Nyumba za kisasa zinapofanyika au kujengwa bila kufuata miongozo ya kitaalamu ule ukisasa hupotea au kudorora sana kwa sababu kukosekana kwa usimamizi makini wenye kutambua umuhimu na sababu ya uwepo wa vipengele husika hupelekea vitu vingi kupuuzwa au kubadilisha na mwisho ile thamani na hadhi ya nyumba yenyewe kudorora sana.

THAMANI YA NYUMBA ZA KISASA HUDORORA SANA PALE MIONGOZI YA
KITAALAMU INAPOACHA KUZINGATIWA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *