MUONEKANO BORA WA NYUMBA YA KISASA PEKEE HAUTOSHI

Kutokana na mapinduzi makubwa kisanifu na kiteknolojia katika ujenzi na hasa katika taaluma ya ujenzi vilivyopelekea kuongezeka kwa ubunifu muonekano wa majengo ya kisasa umekuwa ni wenye kuvutia sana na kila moja kuweza kuwa wa kipekee pasipo kufanana sana kwa kila mradi. Jambo hili limepelekea watu kuvutiwa sana na muonekano na kuweka akili zao zaidi kwenye muonekano na kusahahau vipengele vingine muhimu kwenye jengo.

KUWEKA MAKINI KWENYE MUONEKANO PEKEE NA KUSAHAU VIPENGELE VINGINE NI MAKOSA

Ukiachana na muonekano wa nje wa jengo ambao ni muhimu sana katika kutoa tafsiri ya jengo na usahihi wa kimuonekano kuna vipengele vingine muhimu katika jengo vinavyopaswa kuzingatiwa saa kama vile mpangilio wa ndani ya jengo, ukubwa wa vyumba na nafasi nyingine ndani ya jengo, mpangilio wa mifumo inayopeleka huduma mbalimbali ndani ya jengo, usahihi wa kimpangilio na vipimo vya wima na mlalo, kiasi cha hewa na mwanga asili ndani ya jengo kupelekea kupunguza matumizi ya niashati n.k.,

WEKA UMAKINI KWENYE KILA KITU KATIKA KUTENGENEZA MICHORO YA JENGO LAKO

Ni muhimu sana kwamba wakati ukifikiria muonekano bora wa jengo ujaribu kufikiria na vitu vingine ambavyo utakuja kukutana na uhalisia wake na kuona madhara yake wakati wa kutumia jengo husika ambayo kwa sasa sio rahisi kuonekana na mtu asiye mtaalamu mwenye uzoefu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *