TATIZO LA RAMANI ZA NYUMBA ZA KWENYE MITANDAO.

Kumekuwepo na uuzwaji wa ramani za nyumba mbalimbali za mitandaoni hasa miaka hii ya karibuni na baadhi ya watu wamekuwa wakishawishika kununua kwa sababu zinaonekana zinapatikana kwa bei rahisi kidogo pia. Lakini matatizo yanayoletwa na ramani za mitandaoni ni makubwa sana kiasi kwamba hata huo urahisi wa bei hutaona umuhimu wake tena.

USUMBUFU AMBAO RAMANI YA MTANDAONI ITAKULETEA HUTAONA HATA UMUHIMU WA HIYO GHARAMA RAHISI

Jambo moja la msingi sana la kuzingatia ni kwamba wewe huhitaji kuletewa nyumba bali unahitaji nyumba ambayo utashiriki kuitengeneza. Ni muhimu sana kujua kwamba kila mtu ana vipaumbele tofauti kabisa na mwingine kwa sababu kila mtu ana vitu vyake vya kipekee anavyopenda katika nyumba pia kuna utamaduni tofauti, uzoefu tofauti, hali tofauti za kiuchumi n.k. Huwa ni mara chache sana watu kufanana kabisa juu ya kile wanachokihitaji.

KILA MTU ANA VIPAUMBELE TOFAUTI AMBAVYO RAMANI YA MTANDAONI HAITAKIDHI KWA SABABU HAIJATENGENEZWA KWA AJILI YAKO

Unaponunua ramani ya mtandaoni unainunua kama ilivyo na huwezi kuibadilisha na pale utakapojaribu kuibadilisha vile unavyofikiri wewe mara nyingi utaharibu zaidi na utaona afadhali ungeiacha kama ilivyo kwa sababu kila kitu kimepangiliwa kwa mahesabu ambayo wewe utakuwa huyajui au mpaka au mtaalamu au utumie akili sana kuelewa hasa kwa nini ilifanyika hivyo. Na kwa sababu umeinunua mtandaoni na hakuna mtu wa kuja kukusaidia kuibadilisha vile unavyotaka unaweza kulazimika kuitumia kama ilivyo, kuachana nayo kabisa na kuhesabu hasara au kutafuta mtaalamu ambaye utamlipa fedha nyingi kuliko hata ulizolipia hiyo ramani ili akusaidie kuibadilisha au kuandaa nyingine.

UKIKOSA MHUSIKA WA KUJA KUKUFANYIA MABADILIKO YA RAMANI YA MTANDAONI, AIDHA UTALAZIMIKA KUKUBALIANA NA MAKOSA YAKE AU KUANZA UPYA

Ramani ya mtandaoni inaweza kukuvutia kwa muonekano lakini usahadaike na kuikimbilia kwa sababu utajiingiza kwenye matatizo ambayo utakuja kuyajutia.

MUONEKANO WA RAMANI YA MTANDAONI UTAKUHADAA KUJITUMBUKIZA KWENYE MATATIZO UTAKAYOYAJUTIA

Kama unahitaji ramani ya nyumba usiwe na haraka wala papara, kwa sababu unaenda kuwekeza pesa nyingi sana kwenye mradi husika, unatakiwa kutafuta mtaalamu ambaye mtakaa naye chini mjadili kila kitu kwa marefu na mapana, aweze kukuelewa kwa usahihi, afanye kazi yako kisha muijadili tena kama imetimiza vigezo unavyotaka ndio kisha kazi hiyo imaliziwe kisha hatua nyingine za ujenzi ziendelee.

TAFUTA MTAALAMU AMBAYE MTAONANA NA KUSHIRIKIANA KUANDAA MICHORO YA NYUMBA YAKO

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *