HUWEZI KUNUNUA RAMANI YA KWENYE MTANDAO UKABAKI SALAMA.

Kazi za kitaalamu zina vitu vingi ambavyo kama ukivikiria kwa juu juu sio rahisi kuviona lakini ukija kuingia katika uhalisia ndipo unakutana navyo. Hapa kwa mfano mtaalamu wa kusanifu au kubuni jengo anatakiwa kufika katika kiwanja ambapo jengo husika linajengwa kuweza kuona ni aina gani ya jengo na kwa uelekeo gani linaweza kukaa kwa usahihi, nini cha kuongeza kwenye jengo hilo ili eneo linapojengwa litumike kwa usahihi zaidi na nini cha kupunguza ili kuendana na uhalisia, lakini kwa kutumia ramani ya mtandaoni maana yake hatua hii muhimu inarukwa na pengine hata nafasi ya kujadiliana na mtaalamu juu ya uhalisia huu haitakuwepo ambapo hilo itakuja na madhara makubwa baadaye.

RAMANI INAYOFANYIKA KABLA TAARIFA ZA KIWANJA HAZIJAJULIKANA MARA NYINGI HUJA NA GHARAMA KUBWA BAADAYE

Lakini pia kwa kutumia au kununua ramani ya mtandaoni inamaanisha kwamba suala la ukubwa wa kiwanja na vipimo vyake halitazingatiwa na badala yake kiwanja ndio kitalazimika kupokea ramani ya kutoka kwenye mtandao na kulazimika kukaa katika kiwanja bila kujali madhara yoyote yatakayojitokeza kuhusiana na ukubwa, jiografia au umbo la kiwanja.

RAMANI INAYOTOKEA MITANDAONI INALAZIMISHWA KUENEA KWENYE KIWANJA

Ni muhimu sana kufikiria yote haya ambayo kwa mtu wa kawaida asiye na ufahamu mkubwa wa kitaalamu juu ya changamoto zinazotokana na mpangilio wa kisanifu na mambo mengine muhimu kuhusu ujenzi anaweza kuyatazama kwa juu juu kisha kwenye uhalisia anakuja kukutana na matatizo asiyoweza kuyatatua.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *