RAMANI YA MTANDAONI HAIJATENGENEZWA KWA AJILI YAKO.

Kama nilivyotangulia kusema katika makala zilizopita kwamba kila mtu ana haiba tofauti na vipaumbele tofauti na mtu mwingine sambamba na mtazamo tofauti, matamanio tofauti, uzoefu tofauti, utamaduni tofauti, Imani tofauti na hata kipato tofauti. Haya ni mambo yanayoleta utofauti kati ya tabia ya mtu mmoja na mwingine na hata matokeo tofauti katika kazi zao. Na hii ndio maana nasema kwa uzoefu katika kazi hizi za ujenzi, ni nadra sana ukakuta watu wawili tofauti wamependa kitu kimoja n ahata inapotokea wamekaribiana sana kufanana kwa kile wanachopenda utakuta kuna sehemu ndogo wametofautiana.

UTOFAUTI WA TABIA, IMANI NA UTOFAUTI HUPELEKEA WATU KUTOFAUTIANA HATA KWENYE MACHAGUO NA MATAMANIO

Sasa tunapokuja kwenye suala hili la ramani za mitandaoni, ramani hizi zinatengenezwa kutokana uzoefu tofauti na vipaumbele tofauti vya aidha mteja aliyetengenezewa ramani mwanzoni au mtaalamu mwenyewe aliyetengeneza kadiri alivyofikiri itafaa na mara nyingi utakuta amewaza na kudhania vitu fulani ndio akafanya alichofanya. Vyote hivi sio rahisi viendane na mahitaji yako kwa sababu ya utofauti wa sifa nyingi sana tulizozianisha hapo juu na hivyo unapochukua ramani hiyo ya mitandaoni na kutaka kwenda kuijenga mara nyingi hutaweza kukwepa changamoto hizi na matokeo yake sio rahisi ramani hiyo kukuridhisha ukapata kile haswa unachotaka.

UNAHITAJI RAMANI YA NYUMBA ILIYOTENGENEZWA KIPEKEE KWA AJILI YAKO

Hivyo kwa kuwa ramani hizi za mitandaoni kwani hazijatengenezwa kuendana na wewe wala kuweka mbele ndoto zako na matamanio yako ni maamuzi ya busara zaidi kuachana nazo ili kuepuka kujifedhehesha na badala yake kutafuta mtaalamu ambaye mtashirikiana kufanikisha nyumba iliyotengenezwa kipekee kwa ajili yako.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *