TUMIA RAMANI ZA KWENYE MITANDAO KUONGEZA UELEWA WAKO.

Ili kufanikisha mradi wako uende kwa usahihi sana na kwa namna ambayo utaendelea kufurahia nyumba yake kwa muda mrefu zaidi baadaye unahitaji kushiriki katika kuifanya na sio kushiriki tu bali kufikiri kwa kina kujua hasa unataka kufanikisha nini katika mradi husika. Sasa mwanzoni unaweza usigundue vitu vingi muhimu unavyohitaji lakini kadiri muda unavyokwenda na kadiri unavyolifkiria jengo lako au mradi wako ndivyo utakavyoendelea kugundua vitu zaidi lakini pengine ukiwa umeshafanya kazi kwa kiasi kikubwa.

TUMIA RAMANI ZA MITANDAONI KUPATA UELEWA ZAIDI WA KILE UNACHOTAKA

Hivyo ili mtu uelewe vitu vingi mapema na kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa mradi wako huna budi wewe mwenyewe kufuatilia kazi mbalimbali zilizofanyika zitakazokukumbusha vitu vingi mapema ambapo unapokutana na mtaalamu kujadili mradi huo utakuwa tayari una mengi ya kuzungumza naye na kuweza kugusa maeneo yote muhimu unayohitaji na hivyo kuweza kueleweka kiurahisi.

RAMANI ZA MITANDAONI NI KWA AJILI YA KUJIFUNZA PEKE YAKE KABLA HUJAMUONA MTAALAMU MKAELEWESHANA VIZURI ZAIDI

Sasa moja katika ya sehemu ambayo unaweza kupata mawazo mengi na kuongeza sana uelewa wa mradi husika au yale unayotaka ni mitandaoni, unaweza kuingia mitandaoni kwa lengo la kujifunza na utakutana na vitu vingi, kazi nyingi na maarifa mengi ya kukuwezesha kukumbuka mambo mengi ambayo unaweza kuwa unayahitaji yaongezwe kwenye jengo lako katika kuhakikisha unafanikisha kile hasa unachohitaji na kinachotimiza kusudi lako kwa usahihi zaidi. Hivyo ramani za mitandaoni ni fursa ya kujifunza zaidi na kuongeza uelewa wa kile unachohitaji lakini haipaswa kuchukua na kuzitumia kwani zitakuingiza kwenye matatizo makubwa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *