KUJENGA GHOROFA YA KISASA KIENYEJI NI KUJIANDAA NA MAJUTO.

Ujenzi wa nyumba za ghorofa za kisasa umeshamiri sana na watu wengi zaidi wanazidi kujiingiza kwenye ujenzi wa nyumba za ghorofa kwa sababu kadhaa. Moja ikiwa ni uhitaji wa nyumba yenye vyumba vitu vingi ndani na nyingine ni katika kupunguza matumizi ya eneo kubwa la ardhi.

IDADI YA WATU WANAOJENGA NYUMBA ZA KUISHI ZA GHOROFA IMEONGEZEKA SANA

Hata hivyo wengine wanavutiwa zaidi nyumba ya ghorofa kwa kuona kwamba ni nyumba yenye mvuto na inayopendeza zaidi huku wengine wakipenda tu ule ufahari wa kuwa na nyumba ya ghorofa, na kwa sababu wana uwezo wa kumudu kujenga ghorofa basi wanaona kwa nini wasijenge nyumba za ndoto zao. Hivyo nyumba za ghorofa zinajengwa sana kwa sababu mbalimbali lakini hata hivyo ni kweli nyumba ya ghorofa ina thamani yake ya tofauti hasa endapo imejengwa kwa usahihi na kwa namna inayomvutia mmiliki wake.

WATU WENGINE HUVUTIA NA NYUMBA ZA KUISHI ZA GHOROFA KWA SABABU YA MUONEKANO

Lakini bado kuna changamoto kubwa moja, pamoja na kwamba nyumba za ghorofa zinahusisha gharama kubwa sana kuzijenga, pamoja na kwamba nyumba za ghorofa zinahitaji umakini mkubwa ili kujengwa katika viwango bora bado kumekuwa na ujenzi wa kienyeji ambao unachangia sana nyumba hizi za ghorofa kushindwa kuwa na thamani inayoistahili licha ya kukamilika kwa gharama kubwa.

NYUMBA YA GHOROFA INATAKIWA KUZINGATIA SANA UTAALAMU KATIKA KUJENGWA KWAKO ILI KULINDA HADHI YAKE.

Unapoamua kujenga nyumba ya ghorofa ya kisasa unapaswa kujua kwamba gharama za kitaalamu ni ndogo sana ukijaribu kulinganisha na gharama za ujenzi wa jengo lote, hivyo ni muhimu sana katika kulitendea haki jengo lako na katika kuhakikisha unafikia malengo yako kwa usahihi, basi uhakikishe huduma ya kitaalamu inazingatiwa tangu mwanzo kabla ya michoro ya ramani mpaka mwisho jengo linakabidhiwa baada ya kukamilika. Kwa utaratibu huu utajikuta unafurahia jengo lako tangu mwanzo mpaka kulitumia vinginevyo endapo utaendesha mambo kienyeji utajikuta unajutia sana kwa uharibifu uliofanyika licha ya kutumia pesa nyingi katika ujenzi huo.

Jengo ghorofa la kisasa kitaalamu ili liwe la kisasa kweli kweli.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

8 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *