VIBALI VYA UJENZI NA USAJILI WA MRADI WA UJENZI TANZANIA.
Baada ya michoro ya ramani za ujenzi kukamilika mamlaka husika zimeweka utaratibu wa kufuatilia vibali vya ujenzi ili kuhalalisha mradi husika katika utaratibu wa kisheria. Ambapo kuna aina mbili za mamlaka zinazotoa vibali vya ujenzi zilizogawanyika katika idara mbalimbali. Kwanza kuna kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri ya manispaa au mji husika ambacho ndicho hutangulia kwanza ambapo mamlaka hii ya kutoa kibali cha ujenzi imegawanyika katika idara mbalimbali ambazo michoro ya ramani inapitishwa kwenye kila idara kuangaliwa kama imekidhi vigezo na masharti ndipo iridhiwe kuendelea.
Idara za halmashauri za miji na halmashauri za manispaa ni pamoja na idara ya ujenzi, idara ya mipango miji, idara ya mazingira, idara ya afya n.k, ambazo zote zina taratibu zake ambazo zikishapita na masharti yake ambapo michoro hupitishwa na kusainiwa na wakuu wa idara husika ndio kuruhusiwa kuendelea na mzunguko.
Aina ya pili ya mamlaka ambayo michoro ya ramani hupita ili kupatiwa vibali husika ni kwenye bodi mbalimabli za taaluma zaujenzi ambapo miradi hukaguliwa kama imekidhi vigezo na kuandikishwa kisha kupewa vibali na bodi hizi ambazo kazi yake kubwa ni kukakikisha miradi husika inazingatia utaratibu wa kitaalamu uliowekwa na mamlaka hizi kuhakikisha jengo linafikia viwango vinavyokubalika. Bodi hizi za taaluma za ujenzi ni pamoja na bodi ya wasanifu majengo na wakadiriaji majenzi, bodi ya wahandisi na bodi ya wakandarasi. Bodi hizi hutoa stika maalumu ambazo hupandikwa katika kibao mfano wa tangazo linalokuwepo katika eneo la ujenzi linaloweza kuonekana kiurahisi na huonyesha majina ya kampuni zote ambazo zinahusika kusimamia taratibu za kitaalamu za bodi husika katika mradi.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!