GHARAMA ZA KUPATA VIBALI VYA UJENZI TANZANIA IMEGAWANYIKA MARA MBILI.

Ikiwa unajenga nyumba ya kuishi isiyo ya ghorofa kwa Tanzania huwa unahitaji aina moja ya kibali peke yake ambacho ni kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri ya jiji, manispaa au mji ambapo mradi husika unajengwa. Kibali hiki kinapatikana kwa kuombwa ukiwa umeambatanisha michoro ya ramani iliyopigwa mihuri rasmi pamoja na hati ya kiwanja au taarifa za kiwanja cha eneo husika ambapo mradi huu unajengwa. Gharama za kibali hiki hubadilika mara kwa mara lakini napo gharama hizi hutegemeana na ukubwa wa nyumba mradi wenyewe kwa upande wa mita za mraba zinazojengwa. Kwa gharama sasa imefikia kwamba kwa jengo lenye mita za mraba za wastani wa 250 gharama zake za kibali cha ujenzi inaweza kuwa kwenye wastani wa Tshs 350,000.

GHARAMA ZA VIBALI VYA UJENZI HUBADILIKA MARA KWA MARA

Lakini ikiwa unajenga nyumba ya kuanzia ghorofa moja kwa Tanzania kuna aina mbili za vibali vya ujenzi, ambapo kuna hicho kibali cha ujenzi kinachotolewa na halmashauri ya jiji, manispaa au mji kisha baada ya kukamilisha hicho kuna vibali vinavyotolewa na bodi za taaluma za ujenzi. Vibali vinavyotolewa na bodi za taaluma za ujenzi vinatolewa baada ya kufanya makadirio ya gharama ya mradi husika kisha unalipia kiasi kilichopangwa kadiri ya ukubwa wa mradi kwa upande wa gharama za ujenzi kisha utapewa stakabadhi pamoja na stika yenye nembo ya bodi husika utakayoiweka kwenye kibao cha ujenzi kinachoelezea aina ya mradi na wadau wanaohusika kusimamia mradi huo.

GHARAMA ZA VIBALI VYA UJENZI VINAAMULIWA NA UKUBWA WA MRADI WENYEWE PIA

Baada ya vibali vyote hivi vya ujenzi kukamilika ndipo unapata uhalali wa kisheria wa kuanza kazi ya ujenzi huku ukisimamia na makampuni yaliyosajiliwa kwenye bodi husika ambao watakuwa wanafuata masharti yaliwekwa na bodi husika katika usimamizi huo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *