KUPATA KIBALI CHA UJENZI KWA URAHISI PELEKA MICHORO IKAGULIWE KWANZA.

Katika zoezi la kufuatilia kibali cha ujenzi mara nyingi ni rahisi kukutana na usumbufu unachangiwa pia na urasimu uliopo katika baadhi ya halmashauri ambapo mara nyingi michoro hutolewa kasoro nyingi na kuambiwa haijatimiza vigezo vya kupewa kibali na kwamba unatakiwa kufanya marekebisho kadha wa kadha katika michoro hiyo ili iweze kupitishwa na kufikia kupewa kibali cha ujenzi.

WATU WA KITENGO HUSIKA HALMASHAURI WANA UZOEFU MKUBWA WA KUJUA MAPUNGUFU YALIYOPO KATIKA MICHORO YA RAMANI

Sasa ili kuepuka jambo hili unaweza hata kabla huja-print nakala ngumu ukapeleka michoro yenyewe kwa watu wa vitengo husika kwenye halmashauri ya jiji, manispaa au mji inapojengwa wakaangalia na kujiridhisha kama imetimiza vigezo vyote husika ndipo utoe nakala ngumu ambazo zitagongwa mihuri na kupelekwa halmashauri husika ambapo sasa utakuwa umeepuka usumbufu wa kurudishwa rudishwa sana kwenda kufanya mabadiliko ambayo yangeweza kuonekana mapema na kurekebishwa. Kama ni watu unaelewana nao vizuri unaweza hata kutuma katika mfumo wa nakala tete kupitia barua pepe au hata simu ikaguliwe kukupunguzia usumbufu na kupoteza muda.

WAKIWA WAMESHAIONA MICHORO NA KUIKUBALI INAKUWA KAZI RAHISI KUIPITISHA BILA KUKULETEA USUMBUFU

Hili ni muhimu zaidi kwamba watu mara nyingi huwezi kuwa na mtazamo hasi kwa kitu ambacho ni kipya kwao na pia tafsiri yao inaweza kuwa ina upekee wa aina yao, lakini wanapokuwa wameona tayari na kutoa maoni inamaanisha michoro hiyo haitakuwa mipya tena kwao n ahata kama ni kuitafsiri utakuwa ulishawapa uhuru wa maoni ambao kama waliutoa inamaanisha michoro itakuwa inaendana kabisa na mitazamo yao na kwa kuwa walishakubali kwamba michoro iko sawa au itakuwa sawa baada ya marekebisho watakayotoa basi ni rahisi kabisa wao kuipitisha bila kipingamizi. Jambo hili linaweza kukuokolea muda, gharama na usumbufu mapema kabisa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *