CHANGAMOTO YA KIBALI CHA UJENZI KWENYE MATUMIZI YA KIWANJA.

Mara nyingi watu wamekuwa wakikutana na changamoto sana kwenye kupata kibali cha ujenzi pale wanapopeleka michoro ya ramani za mradi husika katika halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika kutokana na matumizi ya kiwanja kutoshabihiana na lengo la mradi. Kuna kesi nyingine watu wamekuwa wakishangaa zaidi pale ambapo matumizi ya kiwanja yanaweza kuwa ni makazi na mtu akapeleka mradi ambao ni wa makazi lakini bado akazuiliwa na kuambiwa kwamba mradi wake ni wa makazi biashara na sio makazi pekee hivyo hataweza kupewa kibali mpaka afanye marekebisho.

MATUMIZI YA ENEO NI MOJA KATI VIGEZO MUHIMU KUWEZA KUPEWA KIBALI CHA UJENZI

Hili limekuwa likiwagharimu watu wengi muda na hata gharama kwa sababu ya kutokujua utofauti huu au hata kutokufikiria kabisa kuhusu suala la matumizi ya ardhi husika ukilinganisha na aina ya mradi anaotaka kuujenga hapo. Usumbufu ambao utakutana nao kwenye halmashauri ni mkubwa na utakupotezea sana muda na gharama jambo ambalo unahitaji kuanza kujiandaa nalo mapema kabisa wakati unaanza kufikiria kuanza kutengeneza michoro ya ramani.

KUJIANDAA MAPEMA NI MUHIMU SANA ILI KUEPUSHA USUMBUFU NA KUPOTEZA MUDA

Hivyo ni muhimu sana kwamba tangu mwanzo kufuatilia suala la matumizi ya kiwanja na kupanga kwa usahihi au kuanza mchakato wa kutuma maombi wizara ya ardhi kwa ajili ya kubadilisha matumizi ya eneo hilo mapema. Lakini endapo tayari umeshafika mbali na ulishaanza kukosea tangu mwanzoni ni vyema ukaonana na mtaalamu kwa ushauri zaidi kwamba nini hasa kinaweza kufanyika kwa sababu mambo haya huwa yanahusisha vitu vingi ikiwemo hasara za kifedha ambazo mtu anaweza kuingia kwa urasimu uliopo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *