KAMA UNA MPANGO WA KUJENGA NYUMBA KWENYE MAISHA YAKO SOMA HAPA.

Leo nakuja na ushauri huu, ikiwa una mpango wa kufanya mradi wowote wa ujenzi kwenye maisha yako basi anza kutafuta mtaalamu sasa hivi, ukutane naye na kufanya mazungumzo hata kama bado hujaanza kujianda kifedha. Kufanya hivi hakuna gharama kubwa lakini itakusaidia kwa kiasi kikubwa sana na pengine ukafanikisha lengo lako mapema kuliko jinsi ingetokea endapo ungekuwa huna maandalizi kabisa na kukuepushia pia na msongo wa mawazo.

KUNA MAMBO MENGI SANA UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU NYUMBA NA UJENZI WAKE AMBAYO BADO HUYAFAHAMU.

Japo ujenzi unaonekana kama ni kitu cha kawaida kwa sababu watu wamekuwa wakiona ujenzi ukifanyika kila siku tangu wadogo mpaka wamekuwa lakini linapokuja suala la ujenzi watu wengi hawaelewei mambo katika uhalisia. Watu husubiri mpaka pale anapokuwa tayari kujenga ndipo anaanza kufuatilia na kuulizia mambo mbalimbali na wengi hushangaa na kutoamini vitu vingi wanavyoambiwa. Changamoto zaidi ni kwamba mtu unakuta hajajiandaa na vitu vingi vinavyohusisha ujenzi hasa kama inabidi afuatilie baadhi ya mambo kama vile matumizi ya ardhi na vibali vya ujenzi kutoka kwenye mamlaka husika, hili limekuwa linazidi kuwachanganya na kuwapotezea muda ambao pengine wasingeupoteza endapo wangekuwa wamefahamu na kuanza kufuatilia mambo haya mapema kabla hawajasubiri wakati ndio wanataka kujenga.

UKIANZA KUFUATILIA UJENZI WAKATI WA KUANZA KUJENGA UTAKUTANA NA MAMBO MENGI USIYOYAJUA AMBAYO UTATAMANI UNGEYAFAHAMU MAPEMA.

Hivyo ni muhimu sana ikiwa mtu una mpango wa kujenga hata kama ni suala unalotaka kulifanya ndani ya kipindi cha miaka kumi au hata zaidi, ukatafuta mtaalamu sasa akakueleza kwa undani na kwa uwazi nini utatakiwa kufanya ili uweze kuanza kujiandaa mapema lakini pia wewe mwenyewe utakaa kwenye nafasi nzuri ya kuanza kufikiria kuhusu unachokwenda kufanya na utapata mawazo mengi zaidi n ahata kujiandaa kifedha kwa kile unachoelekea kufanya. Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *