UJENZI WA NYUMBA YA KISASA, JIANDAE KUANZIA SASA HIVI USISUBIRI MUDA UFIKE.

Wote tutakubaliana kwamba mara nyingi mtu unapofanya kufanya jambo lolote huwa unakutana na vitu vingi vypya ambavyo ungetamani uvijua mapema ili ufanye maandalizi sahihi jambo ambalo lingekuweka katika nafasi nzuri zaidi kuliko namna ulivyochelewa. Kwa mfano utakuta mtu anasema ningejua hiki kiwanja kitaniletea usumbufu huu ningefanya maamuzi mapema ya kukibadilisha na kile kingine au ningeamua kuhamia kule tofauti na nilivyoamua kuhamia hapa au nisingetumia aina ya utaalamu au malighafi.

UJENZI WA NYUMBA YA KISASA

Mambo yote haya huwa yanajulikana na watu wazoefu ambao wana maarifa na taarifa sahihi lakini wakati huo huo wana uzoefu mkubwa wa kesi kama hizo, ambapo endapo ungekuwa umefanya maandilizi tangu mapema kwa kushirikisha mtaalamu mwenye uzoefu mngekuwa mmejadili suala husika na kulifanyia maamuzi yatakayowaepusha na changamoto ambayo unapitia kwa kutokufahamu maamuzi sahihi ya kufanya kwa wakatis sahihi.

UJENZI WA NYUMBA YA KISASA

Hivyo ili kuepuka majuto ya namna hii pamoja na hasara mbalimbali ni vyema kuanza maandilizi mapema yakupe muda wa kujipanga na kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika mchakato mzima unaotaka kwenda kuufanyia kazi kwa sababu nyumba za kisasa zina mambo mengi na zinahitaji maandilizi muhimu kuliko nyumba holela.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *