HUWEZI KUKWEPA HASARA KWENYE UJENZI WA KISASA KAMA HAKUNA USIMAMIZI WA KITAALAMU.

Jambo ambalo ni lazima litokee karibu mara zote kwenye mradi wowote wa ujenzi ni mabadiliko wakati ujenzi unaoendelea. Hili sio rahisi kukwepeka kwa namna yoyote ile, hata kama mtu unaweza kufikiri kwamba utakuwa makini sana wakati wa kutengeneza michoro ya ramani ili kusiwe na mabadiliko yoyote utashangaa tu yametokea. Kwa hiyo karibu mara zote utakutana na mabadiliko na wakati mwingine mabadiliko yakatokea mara kwa na karibu kila hatua.

MABADILIKO KWENYE MRADI WAKATI WA UJENZI SIO JAMBO LINALOKWEPEKA

Sasa mabadiliko yoyote yanahitaji maamuzi sahihi ili yasipelekee uharibu, na hapa ndipo kosa huwa linafanyika. Kosa hufanyika pale mabadiliko yanapofanyika bila kuhusisha mtaalamu ambaye ataona nini kinachoenda kubadilika na madhara ya mabadiliko haya katika usanifu wa jengo na katika ujenzi pia. Mabadiliko haya yanapofanyika kiholela ndipo huwezi kukwepa uharibifu wa aina mbalimbali na thamani ya jengo lenyewe kupungua kutokana na makosa haya yanayokuwa yamefanyika.

MABADILIKO HAYATAKIWI KULETA UHARIBIFU YANATAKIWA KUONGEZA UBORA

Hivyo jambo la muhimu sana ili kuepuka uharibifu huu ambao ukishatokea huna namna zaidi ya kuingia hasara ya kubomoa tena ili kufanya kazi kwa usahihi unaotakiwa, ni kuhakikisha mradi unasimamiwa kitaalamu ili kukwepa changamoto hizo. Gharama ya hasara hiyo itatengemea na umbali ambao mradi umefika baada ya makosa hayo yaliyofanyika. Epuka kufanya kazi kiholela, epuka hasara zisizo na ulazima.

EPUKA KUFANYA KAZI KIHOLELA KUEPUKA HASARA ZISIZO ZA LAZIMA

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *