CHANGAMOTO KUU YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI.

Mchakato wa kufanikisha kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri ya mji, manispaa au jiji husika umekuwa ukukimbana na changamoto mbalimbali katika hatua zake za kufanikisha kupata. Changamoto hizi zimekuwa za aina mbalimbali kadiri ya vigezo na masharti husika. Lakini changamoto nyingi huwa ni ndogo na zinazotatulika kwa kufanya marekebisho kidogo ya michoro ya ramani husika au kusukuma kwa nguvu zaidi ikiwa ucheleweshwaji uko ndani ya idara za halmashauri ya mji, manispaa au jiji husika.

KUNA CHANGAMOTO NDOGO NA KUBWA KATIKA MCHAKATO MZIMA WA KUFANIKISHA KUPATA KIBALI CHA UJENZI.

Changamoto kubwa ambayo hutokea mara kwa mara na ambayo sio rahisi kutatulika au inayohitaji maamuzi magumu sana ni changamoto ya kiwanja husika kushindwa kutimiza vigezo vya matumizi ya kiwanja kwa mradi unaoombewa kibali. Hapa unakuta matumizi ya kiwanja yameainishwa kuwa ni kwa ajili ya makazi pekee lakini wewe mradi wako unaashiria kwamba ni makazi biashara, hapo utakutana na changamoto kubwa na utakaliwa kupewa kibali cha ujenzi. Sasa kitakachotakiwa hapa ni aidha ubadilishe michoro na kufuata kile ambacho matumizi ya kiwanja yanataka kitu ambacho sio unachohitaji wewe au ubadilishe matumizi ya kiwanja kutoka makazi pekee kuwa makazi biashara, mchakato ambao utakuchukua muda mrefu sana kuukamilisha.

KIGEZO CHA MATUMIZI YA KIWANJA KIMEKUWA NI CHANGAMOTO KUU YA MRADI WA UJENZI KUFANIKIWA KUPATA KIBALI CCHA UJENZI

Sasa unapokutana na changamoto ya namna hii ni vyema kuonana na mtaalamu wa masuala ua ujenzi mkaweza kujadiliana mnafanyaje ili wewe uweze kufanikisha lengo bila kuathiri sana maamuzi yako ya mwanzoni.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *