UJENZI BORA NI MATOKEO YA USHIRIKIANO THABITI.

Tunapozungumzia ujenzi bora tunazungumzia matokeo, lakini matokeo haya yanaletwa na mchakato amabo umepangika vizuri na kujumuisha watu wenye uwezo mkubwa na uzoefu katika fani tofauti za ujenzi. Mchakato huu unapoandaliwa na kupangwa kwa usahihi ndio unaleta matokeo unayoweza kuyaita ni ujenzi bora.

UJENZI BORA NI MATOKEO YA MCHAKATO ULIOPANGIKA KWA USAHIHI

Ujenzi umegawanyika katika pande kuu mbili amabazo, moja ni upande wa washauri wa kitaalamu ambao ndio wanatoa miongozo yote kuhusu ujenzi na mara nyingi wanachoamua wao ndicho kinachotekelezwa kwa sababu ndio wataalamu wenye taaluma kuhusu ujenzi, kazi yao kubwa ni kutoa maelekezo na kusimamia usahihi wa utekelezaji wa maazimio hayo. Upande wa pili ni upande wa wakandarasi ambao kazi yao kubwa ni kufanya utekelezaji wa mradi kwa maelekezo kutoka kwa washauri wa kitaalamu. Wakandarasi wana kazi kubwa ya kuhakikisha kila kilichoamuliwa na washauri wa kitaalamu kinaingizwa kwenye utekelezaji kadiri ya kilivyoamuliwa na wanapaswa kuhakikisha vyote vimefanyika kama ilivyoamuliwa.

UJENZI BORA UNATAKA USHIRIKIANO THABITI

Sasa ujenzi bora ni pale ambapo kuna ushirikiano mkubwa na thabiti kabisa kati ya washauri wa kitaalamu na wakandarasi kupitia vikao vya mara kwa mara ambavyo ndivyo vinahakikisha viwango ni vya hali ya juu na kutatua changamoto zote zinazojitokeza.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *