MAKABIDHIANO KATI YA MTAALAMU ALIYEFANYA MICHORO YA RAMANI NA FUNDI AU MKANDARASI.

Imekuwa kawaida kwa watu kutafuta namna ya kukamilisha hatua ya kutengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wake wa ujenzi wakati mwingine wengine wanadiriki hata kuiba au kuchukua mitandaoni bila kujali madhara makubwa na hasara inayoambatana na kupata ramani bila kuhusika kwa mtaalamu wa usanifu. Kwa watu wengi wakishakamilisha kupata michoro ya ramani kwa ajili ya ujenzi bila kujali ameifanikisha kwa njia gani moja kwa moja huwa anaanza kutafuta mafundi au wakandarasi na kuwakabidhi michoro kwa ajili ya kuanza bila kumhusisha au kumshirikisha mtaalamu aliyefanya michoro kwa ajili ya kukabidhiana na kupeana maelekezo ya mambo muhimu katika michoro na ujenzi. Hili ni kosa kubwa na mara nyingi huja na madhara yake, karibu miradi yote ambayo hakuna mawasiliano kabisa kati ya mtaalamu aliyetengeneza michoro ya ramani na mkandarasi aliyejenga hutokea changamoto kubwa au ndogo kadiri ya uelewa, uzoefu na uwezo wa wahusika.

MAKABIDHIANO YA MICHORO YA RAMANI ZA UJENZI

Kwa maana hiyo basi, ni muhimu sana kabla ujenzi wa mradi husika haujaanza baada ya mkandarasi au fundi kupatikana wakakutana na mtaalamu aliyefanya michoro wakajadili kwa kina na hata kuandika orodha ya mambo muhimu ya kuzingatia na kuweza kuafikiana kwa yote yanayokwenda kufanyika ndio kisha ujenzi wa mradi husika kuanza. Hili litasaidia kurahisisha sana kazi ya ujenzi na kupunguza makosa na kuondoa utata uliopo kwenye baadhi ya maeneo. Ikitokea kwa kesi ambayo aliyefanya michoro hawezi kupatikana kabisa hata kwa simu au kwa sababu nyingine zozote au kwa sababu maalumu hawezi kushirikishwa kinachoendelea baada ya kukamilisha kutengeneza michoro ya ramani, basi ni muhimu akatafutwa mtaalamu mwingine wa usanifu kama huyo akajaribu kuisoma ramani husika na kuelewa kwa kadiri atakavyokuwa ameielewa kisha kukaa chini na mkandarasi wakaijadili na kukubaliana kinachokwenda kufanyika na kama kuna changamoto wakatafuta namna ya kuzitatua.

MJADALA NA MAKABIDHIANO YA MICHORO YA RAMANI ZA UJENZI

Hata hivyo mtaalamu aliyetengeneza michoro ndio wa muhimu sana katika kufanya makabidhiano haya kwa sababu yeye ndiye anayeelewa haswa kile alichofanya kuliko kuleta mtu mpya ambaye sio rahisi aelewa kwa asilimia 100% lengo na nia ya mtaalamu aliyefanya kazi hiyo, lakini kama imeshindikana kabisa kupatikana aliyefanya au kwa sababu zozote zile hatakiwi tena kushirikisha basi huyu mwingine anakuwa ni wa muhimu sana pia.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *