LENGO LA MRADI AU JENGO HUSIKA LIJULIKANE NA KUZINGATIWA

Lengo la jengo anayelijua angalau kwa usahihi zaidi ni yule mteja mwenye jengo. Lengo la jengo ni lile kusudi na matamanio ambayo mteja husika ameweka na anayoyatarajia kwenye mradi wa jengi husika. Kwa mfano kwa mradi wa makazi, lengo la jengo linaweza kuwa ni mjumuisho wa utamaduni wa mteja husika, tabia yake, vitu anavyopenda, idadi ya watu na aina ya watu anaotegemea kuishi nao katika jengo hilo n.k.,. Kutokana na mambo kama hayo mteja atakuja na mapendekezo yake yanayoendana na orodha ya mambo hayo kisha kueleweshana kwa usahihi na mtaalamu wa usanifu wa jengo kwa namna ambayo itamridhisha mteja kwa kiwango cha kabisa kadiri inavyowezekana kitaalamu.

LENGO LA MRADI WA JENGO HUSIKA LINAPASWA KUWA MWONGOZO KATIKA SHUGHULI ZOTE ZA KITAALAMU HASA WAKATI WA KUANDAA MICHORO

Hivyo katika kufanya kazi yale malengo ya mteja ndio yanayotakiwa kupewa kipaumbele zaidi katika kufanya maamuzi ya kwenye usanifu. Kwa mfano labda mteja ni mtu mwenye kupenda magari na anamiliki magari mengi ambayo hubadilisha mara kwa mara, hapa unajua kabisa kwamba kutahitajika eneo kubwa zaidi la kuegesha magari kiasi kwamba hata kama ukubwa wa eneo hauruhusu ni lazima utafikiria kuongeza eneo hata chini ya ardhi ili kutimiza lengo hili. Au ukijua kwamba mteja anavutiwa na aina fulani za urembo na mipangilio utahitaji ufahamu kiundani kile hasa kinachomvutia zaidi na kuweka malengo ya kufanya kwa ubora zaidi. Au labda mteja ni mtu anayeishi na familia kubwa yenye mchanganyiko wa watu utajua kwamba ni vitu gani vya kuvipa kipaumbele zaidi kwa namna utamaduni wa eneo husika unaenda kufanya kazi. Kama jengo ni la biashara nalo huwa na malengo mbalimbali kadiri mradi husika ulivyofikiriwa na kubuniwa kulingana na namna biashara inavyohitaji.

LENGO LA MRADI WA JENGO LIKIZINGATIWA HULETA MATOKEO YANAYORIDHISHA KWA PANDE ZOTE

Lengo la mradi linapokuwa wazi linarahisisha sana kazi kuanzia ya usanifu mpaka ujenzi na mwisho wa mradi mteja anakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuridhika na kazi iliyofanyika na kutimiza malengo yake.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *