MPANGILIO WA NGAZI NA LIFTI KWENYE JENGO.

Jengo linapomalizika kujengwa hutumiwa na watu wengi mbalimbali na aina tofauti tofauti kiasi kwamba hata aliyefanya kazi husika ya ujenzi huenda hakuwahi kuwadhania, hii ni kwa sababu matumizi yanayokuwa yamezungumzia mwanzoni huenda yakaongezeka sana zaidi ya ilivyokuwa inadhaniwa mwanzoni au hata kubadilika kabisa wakati mwingine. Hivyo kuna vitu ndani ya majengo vinapaswa kupangiliwa kwa namna ambayo vitaweza kutumika kwa urahisi na mtu yeyote bila kupoteza muda wala usumbufu mwingine wowote kwa watu wengine.

ENEO LA NGAZI NA LIFTI NI MUHIMU KUKAA ENEO LA WAZI LINALOONEKANA KIURAHISI MTU ANAPOINGIA

Hii inahusisha mpangilio wa vitu kama ngazi au lifti ambapo mtu anaweza kufika kwenye jengo hasa kwa majengo makubwa yenye vitu vingi, ambapo anapofika moja kwa moja anahitaji kwenda kwenye sakafu za juu za ghorofa tena akiwa na haraka sana na ni mgeni kabisa kwenye jengo husika, anatakiwa kwenda moja kwa moja bila kupoteza anahitaji kupata huduma ya kupanda juu kiurahisi na kwa haraka bila usumbufu. Na hapo ndipo unapoona umuhimu mkubwa wa mpangilio sahihi wa eneo la ngazi na lifti ya jengo kwamba linatakiwa kuwa rahisi kuonekana na karibu na eneo kuu la kuingilia ikiwezekana pamoja na alama za kuonyesha eneo husika ikiwa jengo hilo ni kubwa sana. Usumbufu huwa na mkubwa sana na kero kwa watumiaji wa jengo pale eneo la ngazi na lifti kwa ajaili ya kupanda kwenye sakafu za juu za jengo linapokuwa halionekani kiurahisi kiasi kwamba mpaka mtu akutane na usumbufu wa kuelekezwa na pengine eneo husika kuwa limejificha sana.

USUMBUFU MKUBWA HUJITOKEZA ENEO HILI LINAPOKUWA LIMEJIFICHA SANA

Mpangilio wa huduma hizi ni kati ya mambo muhimu sana kujadiliwa mapema kabisa mwanzoni mwa mradi, lakini kwa jengo ambalo labda limekuja kutaka kuwekewa lifti baadaye au hata ngazi itapaswa suala hili la ukaribu na eneo la kuingilia au urahisi wa kuonekana kutokea eneo la kuingilia lipewe kipaumbele cha kwanza.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *