MKOPO WA NYUMBA(MORTGAGE)

Mara kwa mara watu wamekuwa wakiniuliza endapo wanaweza kupata aina ya mkopo wanaoweza kuumudu kwa ajili ya kuendeleza eneo la ujenzi alilonalo au hata kupata mwekezaji ambaye wanaweza kuingia ubia wa pamoja waweze kuendeleza eneo kwa kujenga jengo la biashara kwa makubaliano yenye manufaa kwa pande zote mbili. Japo mikopo ya nyumba ipo ya aina nyingi lakini mkopo nafuu na rahisi ni “mortgage” ambayo unachukua mkopo wa nyumba na kujenga au kununua nyumba kisha unakabidhiwa na kuanza kuitumia lakini hati ya nyumba inaendelea kumilikiwa na benki au taasisi ya fedha iliyokupatia mkopo mpaka pale utakapomaliza kulipa mkopo huo ndipo unakabidhiwa umiliki wake.

UNAPASWA KUFAHAMU VIGEZO NA MASHARTI YA TAASISI MBALIMBALI ZA KIFEDHA KUJUA TAASISI IPI INAWEZA KUWA INAENDANA ZAIDI NA NAFASI ULIYOPO

Hata hivyo kwa nchi yetu ni benki chache zinazotoa mkopo wote wa nyumba kwa pamoja katika mazingira ambayo dhamana ni mshahara peke yake lakini kama ukiweza kuwa katika nafasi nzuri na kujitahidi kujiongeza kufikia masharti wanayotaka ikiwa ni pamoja na kumiliki akaunti katika benki husika utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mkopo huo. Jambo la msingi sana ni kuwa na mpango unaoeleweka na unaouzika hasa kama jengo unalotaka kujenga ni la biashara na ikibidi uwe pia tayari na michoro iliyoambatana na nyaraka za makadirio ya gharama za ujenzi husika. Kila benki au taasisi ya fedha ina taratibu zake na masharti yake ambapo kuna nyingine zinatoa kiasi cha fedha na nyingine zinaweza kugharamia mradi mzima kadiri ya manufaa na mafanikio yanayoonekana kwenye mradi husika.

NI BENKI CHACHE NCHINI ZINAZOTOA MKOPO KAMILI WA NYUMBA KWA UTARATIBU WA (MORTGAGE)

Jambo la muhimu ni kufuatilia kujua uko kwenye nafasi gani kuweza kupata mkopo au unatakiwa kujiongeza kiasi gani kuweza kutimiza vigezo na kufanikisha lengo lako.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

10 replies
  1. Thomas maguncho ikwabe
    Thomas maguncho ikwabe says:

    Nilihitaji kujua benki gani zinatoa mkopo wa ujenzi kwetu hapa maana nina kiwanja changu kina hati nimejemga na kupaua lodge nimepungukiwa hela ya finishing nitachelewa nilitamani kupata nimalizie halafu nilipe pole pole

    Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *