MIKOPO YA UJENZI WA NYUMBA TANZANIA (MORTGAGE), INAPATIKANA.
Mikopo ya nyumba aina ya “mortgage” imekuwa ni huduma adimu sana kupatikana kwa nchi yetu ya Tanzania ukilinganisha na nchi zilizoendelea ambapo mikopo ya aina hii ni mingi sana na ni maarufu sana pia. Kwa wasioelewa vizuri “mortgage” ni aina ya mkopo wa nyumba ambapo taasisi ya kifedha inakukopesha fedha kwa ajili ya kununua, kukarabati au kujenga nyumba endapo umetimiza vigezo na masharti yao kisha wanashikilia hati yako ya kiwanja na kumiliki kisheria mpaka utakapomaliza kulipa mkopo husika ndipo watakurudishia na kukukabidhi nyaraka za umiliki na dhamana inaweza kuwa ni mshahara wako. Ulipaji wa mkopo unaweza kuchukua mpaka miaka 15 hadi 20 kutegemea na kiasi ambacho umeamua utakuwa unalipa kila mwezi au endapo utaamua kulipa kwa haraka itachukua muda mfupi.
Benki nyingi Tanzania hazitoi aina ya mikopo hii ya nyumba “mortgage loans” na kwa zile zinazotoa zina masharti mengi magumu na sio rahisi sana bila kumfuatilia mtu kwa kina na kujiridhisha kwamba anaweza kulipa bila mashaka yoyote hasa kwa watu ambao hawana dhamana kuweka za kutosha kuwawishi. Taasisi ya kwanza na pekee Tanzania ambayo inajihusisha moja kwa moja na mikopo ya nyumba ni “First Housing Finance(T) Limited” ambayo iko kwa ajili ya aina hii ya mikopo ya nyumba peke yake. Taasisi hii ya kifedha ina masharti yake kadhaa na riba yake ya mkopo kwa mwaka ni asilimia 16% ambapo dhamana yako inaweza kuwa ni mshahara wako na kiasi utakachokuwa unarudisha kitategemea na ukubwa wa mkopo uliochukua. Wanatoa mikopo ya kununua nyumba, kukarabati nyumba na hata kujenga nyumba kadiri ya uhitaji wa mteja husika. Masharti yao ni kwamba unatakiwa kuwa na hati ya kiwanja pamoja na nyaraka zote za ujenzi ikiwemo michoro yote ya ramani, kibali cha ujenzi na makadirio rasmi ya bajeti ya mradi husika na baada ya hapo taasisi itakugharamia asilimia 80% ya gharama za ujenzi, japo kunaweza kuwa na mazungumzo zaidi baada ya kufahamiana vizuri.
Kwa watu wengi ambao wamekuwa wakijaribu kufuatilia mikopo ya nyumba (mortgage loans) kwenye mabenki mbalimbali na kukutana na changamoto nyingi unaweza kujaribu kuwacheki hawa “First Housing Finance” kupata uzoefu kutoka kwao pia.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!