WATU WANAOHUSIKA KUFANYA MAAMUZI KWENYE MRADI WA UJENZI

Kutokana na kutokufahamu taratibu na madhara yanayoweza kusababishwa na ufanyaji wa maamuzi kiholela kwenye mradi wa ujenzi, imekuwa jambo la kawaida kwa watu kujifanyia maamuzi kwenye mradi wa ujenzi vile watakavyo. Hili limekuwa linakuja na gharama kubwa kwa sababu watu hawa wamekuwa wakifanya maamuzi wakiwa hawana taarifa za kutosha wala uzoefu na utaalamu wa jambo husika zaidi ya mtazamo binafsi ambao unakosa uelewa mpana wa vitu vingi juu ya mradi husika na mwisho maamuzi yao yanaishia kuwa majanga makubwa kwa mradi wenyewe. Kila mtu anaweza kuona mambo kwa mtazamo wake na kufikiri ndio sahihi lakini inahitaji mkusanyiko wa taarifa nyingi, uzoefu na hata kanuni mbalimbali za kitaalamu kuweza kutoa maamuzi sahihi na yanayozingatia malengo na hali halisi ya mradi.

MAAMUZI YANAPOFANYWA NA WATU SAHIHI MRADI UNA NAFASI KUBWA YA KUFANYIKA KATIKA VIWANGO VYA JUU VYA UBORA

Hivyo watu pekee wenye mamlaka ya kufanya maamuzi katika mradi wa ujenzi ni kwanza mteja wa mradi husika, pili ni mshauri wa kitaalamu anayehusika na mradi husika na tatu mamlaka zinahusika kudhibiti taratibu mbalimbali za ujenzi. Mteja wa mradi au mwakailishi wa mteja wa mradi wa ujenzi atafanya maamuzi lakini atashauriana kwanza na mshauri wa kitaalamu au washauri wa kitaalamu kabla maamuzi yake hayajaingizwa kwenye utekelezaji na pengine yatahitaji kuboreshwa ndipo yaingizwe kwenye utekelezaji. Mtu mwingine ambaye ndiye mwenye jukumu kuu la kufanya maamuzi na maamuzi yote yanapaswa kupitia kwake ni mshauri mkuu wa kitaalamu wa mradi husika ambapo hufanya maamuzi mengi ya mradi yanayotokea mara kwa mara kutokana na mambo mbalimbali yanayojitokeza. Mshauri mkuu wa kitaalamu ataandika kila kitu kinachoendelea kwenye na kuhakikisha kinafanyika kwa namna ambayo inaendana na malengo ya mradi na kufuata kanuni sahihi za kitaalamu. Mtu mwingine mwenye sifa za kufanya maamuzi katika mradi wa ujenzi ni mamlaka za ujenzi zinahusika kudhibiti na kusimamia maadili sahihi katika ujenzi ambapo mamlaka hizi kupitia wataalamu wao wanahakikisha sheria na taratibu zote zilizowekwa na mamlaka zinafuatwana ikiwa hazikufuatwa watu wa mamlaka husika watafanya maamuzi kadiri ya sheria inavyowataka juu ya mradi husika.

MAMLAKA ZA UDHIBITI WA MIRADI YA UJENZI ZINAFANYA MAAMUZI KUHAKIKISHA MIRADI INAFUATA TARATIBU ZOTE ZILIZOWEKWA KISHERIA

Ikiwa watu sahihi pekee ndio watafanya maamuzi katika mradi wa ujenzi basi itapunguza sana changamoto, migongano na mivutano itakayoepusha uholela na uharibifu ambao mara nyingi hupelekea hasara.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *