UNAWEZA KUBADILISHA NYUMBA YAKO KUWA GHOROFA

Uwezo wa mtu kiuchumi mara nyingi huwa unaendelea kukua kutokea chini kwenda kwa sababu muda nao ni moja ya sababu za kipato cha mtu kuongezeka ikiwa mtu huyo anafuata kanuni sahihi za mafanikio. Watu wengi hujenga nyumba zao za kuishi au hata aina nyingine za nyumba kadiri ya kipato chao kinavyoruhusu kwa wakati husika, lakini baada ya muda au miaka michache baadaye kipato huongezeka sana na watu hao hujikuta wanahitaji aidha nyumba kubwa zaidi au kuhitaji nyumba ya hadhi ya juu zaidi. Mara nyingi katika hatua hii watu hununua kiwanja eneo jingine na kuamua kujenga nyumba nyingine kubwa zaidi na ya kifahari zaidi kadiri ya ndoto zao. Lakini sio watu wote hupenda kuhama eneo analoishi, wengine huhitaji kubaki eneo lile lile lakini wakihitaji nyumba kubwa zaidi nay a kufahari zaidi lakini wengi hufikiri ni vigumu kubadili nyumba anayoishi kuwa bora zaidi, yenye hadhi ya juu zaidi nay a kifahari zaidi na hasa kuwa ghorofa kutoka kuwa nyumba ya chini.

NYUMBA YA KAWAIDA INAWEZA KUFANYIWA MABADILIKO KADIRI YA UHITAJI WA MTEJA KWENDA KUWA GHOROFA

Inawezekana kabisa badala ya kuhamia eneo jingine ikiwa unapendelea zaidi kubaki hapo hapo ukaibadilisha nyumba yako kutoka kwenye nyumba ya kawaida na kuwa nyumba ya ghorofa. Kitakachofanyika ni italazimu kuitemebelea nyumba husika, kuchukua vipimo kisha kujadili mabadiliko husika kwa kina kuhakikisha kinapatikana kile hasa kinacholengwa. Baada ya hapo mtaalamu ataenda kukaa chini na kutengeneza kile ambacho kinatazamiwa huku wakishirikiana wataalamu wote ambao ni muhimu katika mabadiliko ya jengo mpaka mfumo mzima wa mihimili. Mfumo wa mihimili utapelekea kutambulisha nguzo mpya maeneo muhimu kuongeza maboriti pamoja na urefu wa nyumba kuhakikisha viwango vya ubora katika mifumo ya mihimili na viwango sahihi vya majengo kisanifu vinazingatiwa. Mabadiliko haya yatakuja na mwonekano mpya na wa kipekee kabisa kiasi kwamba mtu anaweza kudhani yuko eneo tofauti na alilokuwa mwanzo na kama utaalamu utakaotumika ni wa viwango sahihi jengo linaweza kupendeza na kuvutia sana kimwonekano na hata ndani ya jengo kukawa na mabadiliko yanayoweza kuongeza sana uhuru wa kimatumizi.

KUBADILI NYUMBA YA KAWAIDA KUWA GHOROFA MABADILIKO MAKUBWA HUWA YAPO KWENYE KUONGEZA MATUMIZI NA KUIMARISHA MIFUMO YA MIHIMILI

Kufanya mabadiliko makubwa kwenye jengo ni kazi inayohitaji umakini na utaalamu mkubwa ikiwa inahitajika kufanyika katika viwango sahihi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *