KUJENGA NYUMBA YA MAKAZI NI ASILI YETU BINADAMU JENGA NYUMBA YA KISASA.

Watu wengi wamekuwa na hamu na hamasa ya kumiliki nyumba zao za kuishi tangu wakiwa na umri mdogo kabisa, wengine wamekuwa na ndoto hizo tangu wakiwa shule ya msingi. Sio dhambi wala sio jambo la ajabu mtu kutamani kujenga nyumba yay a makazi, ni jambo la kawaida kabisa na ni asili yetu binadamu. Utafiti wa kihistoria unaonyesha kwamba binadamu wameanza kujenga makazi ya kuishi kwa maelfu ya miaka nyuma kabla hata historia haijaanza kuwekwa kwenye kumbukumbu. Lakini pia kuna mabaki ya makazi ambayo yamepatikana duniani kote na wanaakiolojia ambayo tafiti za kisayansi zinaonyesha kwamba makazi hayo yamekuwepo tangu miaka 12,000 iliyopita na mengine hata kabla ya hapo. Hii ni ishara kwamba ni asili ya binadamu kujenga makazi bora na sahihi kwake kuishi na pia ni hitaji muhimu la msingi kwa binadamu.

NYUMBA YA KISASA YA MAKAZI YA WATU KARNE YA 21

Kwa hiyo kama watu wameanza kujenga makazi ya kuishi tangu mwanzo wa zama za niolithiki zaidi ya miaka 12,000 iliyopita ambapo kulikuwa na changamoto nyingi sana huku teknolojia ikiwa bado ni duni kabisa basi wewe binadamu wa karne ya 21 ambaye umezaliwa nyakati bora sana ambazo teknolojia imekuwa bora kuliko wakati wowote ule unastahili kujenga nyumba bora sana ya kisasa ya kuishi. Kwa nyakati za sasa una kila kitu na kila sababu ya kujenga nyumba bora ya kisasa. Kwa uzoefu wangu katika sekta ya ujenzi ni kwamba kila mtu akiamua na kujikana mwenyewe ana uwezo wa kujenga nyumba bora ya makazi yake, kitu cha msingi anachotakiwa ni kuweka juhudi kubwa sana katika kazi na biashara zake, kuwa na ndoto ya kufanikisha mradi wa nyumba yake binafsi na kuwa na imani isiyoyumba wala kutetereka kwamba anaenda kufanikisha ujenzi wa nyumba yake hiyo na kuweka muda maalumu wa ni lini atakuwa amefikia ndoto yake hiyo kisha kufanya kazi kwa bidii sana bila kuchoka wala kukata tamaa. Inaweza kuchukua hata miaka kumi au zaidi lakini ukiweka “focus” na kujituma vya kutosha ni suala la muda tu utafanikisha ndoto yako hiyo kubwa na muhimu. Itakuwa ni aibu kwa sisi binadamu wa karne ya 21 kuzidiwa akili na binadamu wa zama za kale kabisa walioweza kufanikiwa kujenga makazi ya kuishi, sisi binadamu wa karne ya 21 tunapaswa kufanya mambo makubwa kuliko binadamu wa zama nyingine zozote kwa sababu tuna taarifa za kutosha kabisa kutoka kwenye kila zaman a tumekusanya maarifa na teknolojia zote tangu zama za kale kabisa.

MAKAZI YA BINADAMU WA ZAMANI ZAIDI TAKRIBAN MIAKA 12,000 ILIYOPITA

Kujenga nyumba bora ya makazi kwa ajili yako na familia yako ni kati ya mambo yatakayokupa utulivu mkubwa wa akili na kurudhika na familia kupata utulivu na kuzidi kujiamini kwani hakuna mahali bora kama nyumbani kwako.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *