KUBADILI NYUMBA YOYOTE YA KAWAIDA KUWA GHOROFA

Mahitaji ya maisha yanabadilika kila siku na kitu ambacho mtu alifikiri kitamfaa miaka mitatu au mitano iliyopita leo kinaweza kuwa hakimtoshelezi tena. Uhalisia huu katika ujenzi wa nyumba hasa za makazi umesababisha watu wengi kujikuta wakihitaji nyumba kubwa yenye nafasi zaidi baada ya miaka kadhaa baadaye kutokana na mahitaji kubadilika au kuongezeka. Baadhi ya watu ambao pia kipato huwa kimeongezeka wamejikuta wakihitaji kupata nafasi zaidi na vyumba zaidi ndani ya nyumba lakini sio kwa kujenga eneo jingine nyumba kubwa zaidi bali kwa kuongeza ile iliyopo iweze kumudu mahitaji yaliyoongezeka bila kuhama eneo husika. Hili ni suala ambalo watu wengi wamekuwa wakiwa na mashaka kama ni suala linalowezekana au litashindikana na kupelekea kuharibu kilichopo au kusababisha majanga.

NYUMBA YOYOTE YA KAWAIDA INAWEZA KUBADILISHWA KUWA GHOROFA LAKINI INAHITAJI UTAALAMU NA UMAKINI

Mchakato wa kubadili nyumba ya kawaida kwenda kuwa ghorofa ili kuwa huru kupata nafasi ya kutosha ni jambo linalowezekana kabisa kitaalamu lakini kwa kuzingatia mambo maalum. Kwanza kabisa itahitaji mtu kutembelea nyumba husika ili kuweza kujua namna ya kuweka yale mahitaji muhimu bila kuharibu mpangilio na muonekano uliopo. Kwa mfano ili kupanda juu kutahitajika kuwe na ngazi na hivyo itahitajika lipatikane eneo ambalo ngazi itakaa ambalo inabidi liwe ni eneo kubwa linalopatikana ndani ya nyumba kwa sababu ngazi ni sehemu inayogharimu eneo kubwa. Ikiwa haijapatikana sehemu ya kutosha kuweka ngazi ndani ya jengo husika italazimu kubomoa chumba au sehemu ya chumba ili kupata sehemu sahihi ya kuweka ngazi ambayo itakuwa inaendana na mpangilio sahihi wa ndani ya jengo na kufikia sehemu sahihi tarajiwa bila kuathiri sana mpangilio wa vitu vingine ndani ya nyumba hiyo. Pia kutahitajika mpaka wa ukanda wa vitu vinavyoendana pamoja na muonekano sahihi ambao hautaharibu taswira na muonekano wa jengo husika. Jambo lingine muhimu la kuzingatia ni mpangilio wa nguzo zinazobeba ghorofa ya juu ambao hautaathiri mzunguko na mpangilio wa nafasi ndani ya nyumba ya chini, na hili pia huhitaji mahesabu sahihi ili kuepuka kuweka nguzo sehemu isiyo sahihi na kuharibu mwonekano.

MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA KWENYE KUBADILI NYUMBA YA KAWAIDA KUWA GHOROFA NI MUONEKANO NA UIMARA

Kabla hujaamua kama nyumba yako inafaa au haifai kubadilishwa kuwa ghorofa ni vyema ukamwita mtaalamu mkajadili kwa kina na kupata uhakika wa kile unachofikiria ili kuweza kufanya maamuzi sahihi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *