RANGI ZA NYUMBA LADHA YAKE IKO KWA MTU BINAFSI LAKINI BAADHI YA RANGI ZINA UPEKEE.

Moja kati ya maeneo ambayo huchanganya sana watu ni kwenye eneo la rangi, ambapo swali gumu kujibiwa huwa ni rangu gani inapendeza zaidi ikipakwa kwenye nyumba au ni rangi gani sahihi kupaka kwenye nyumba. Sintofahamu hii ya ni aina gani ya rangi inapendeza ikipakwa kwenye nyumba inatokana na ukweli kwamba uzuri wa kitu unatafsiriwa kupitia hisia za mtu juu ya kitu hicho an hisia za mtu zina historia ndefu ya asili yake na malezi aliyopitia na hasa vitu alivyozoea na kuamini na kutengeneza maana ya vitu gani vina thamani zaidi ya vitu vingine. Hivyo katika suala hili sintofahamu ni kubwa na inabaki kuwa tafsiri ya mhusika mwenyewe, lakini hata hivyo kazi yoyote ikifanyika kwa viwango vya juu hupendeza bila kujali rangi au aina ya vipengele vingine vilivyotumika.

IKULU YA MAREKANI “WHITE HOUSE” IMETAWALIWA NA RANGI NYEUPE

Hata hivyo pamoja na kila mtu kuwa na mtazamo tofauti juu ya rangi gani yenye ladha nzuri zaidi ya rangi nyingine lakini kuna rangi ambazo zimeonekana katika historia kuwa na hadhi ya tofauti na rangi nyingine kutumika katika majengo au maeneo mengine yenye hadhi za tofauti. Rangi inayoongeza kwa kuwa na hadhi ya kifalme ni rangi nyeupe ambapo inapotawala kama imepangiliwa kwa usahihi huonyesha hadhi ya tofauti mara nyingi na huweza kuleta picha ya kwamba ni eneo ambalo lina umakini wa tofauti n ahata kutumiwa na watu wa hadhi ya juu sana na waliostaarabika sana. Kuna rangi nyingine kama vile nyekundu ambayo mara hutumika kwa sababu maalum hasa kwa upande wa mambo ya imani, mapenzi na tafsiri nyingine za kijamii na kitamaduni. Rangi nyeusi japo kwenye majengo haitumiki sana lakini nayo hutumika kwa sababu maalumu peke yake. Rangi nyingine kama blue, kijani n.k., huweza kutumika katika mchanganyiko maalumu unaoleta ladha ya tofauti na ya kipekee kwa kuongezewa kwenye baadhi ya maeneo kama kwenye mikanda, riboni, maandishi, n.k.,

KWA MAENEO MENGI RANGI NYEUPE IMEKUWA NI ALAMA YA MAMLAKA NA UTAWALA

Pamoja na tafsiri zote za rangi na michanganyiko ya rangi bado tunasema mwisho wa siku kila aina ya mpangilio unaweza kuleta matokeo na tafsiri ambayo inaweza kupendwa kadiri ya ubunifu wa namna ilivyotumika na kufanyika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *