USIKUBALI KAZI YA UJENZI ILIYOFANYWA CHINI YA KIWANGO.

Kazi yoyote ya ujenzi ambayo haina usimamizi unaofuata taratibu sahihi ubora wake unabaki kutegemea busara, nidhani na uwezo wa fundi husika. Changamoto kubwa ni kwamba watu wengi wanaweza kufanya kazi yenye ubora pale tu wanapolazimika kufanya hivyo mara nyingi wanapokuwa chini ya usimamizi madhubuti. Watu hawa wana uwezo wa kufanya kazi kwa viwango vya juu lakini hawana nidhamu hiyo wala hawaoni umuhimu huo mpaka pale inapokuwa ni suala la lazima kwao au hawana namna wala ujanja bali kufanya kazi yenye ubora ndipo wanapofanya. Usimamizi sahihi unafahamu suala hili na mara zote huhakikisha viwango tarajiwa vinafikiwa.

VIWANGO SAHIHI VYA UJENZI VINAPASWA KUFIKIWA VINATAKIWA KUJULIKANA KABLA KAZI YENYEWE HAIJAANZA

Ikiwa umekutana na watu wa namna hii au watu wowote ambao huna uhakika na nidhamu yao katika kazi jambo la kwanza ni kuhakikisha kwamba kuna viwango ambavyo wanawekewa katika kazi ambavyo watalazimika kuvifikia pamoja na kuweka mhusika wa kufanya ufuatiliaji kuhakikisha kwamba viwango husika vinafikiwa kama inavyotarajiwa. Kwa sababu utakuwa umeweka masharti hayo tangu mwanzoni hupaswi kukubaliana na sababu yoyote ya kazi kufanyika chini ya vile mlivyokubaliana isipokuwa tu kama kuna jambo ambalo walihitaji ulikamilishe ndio waweze kuendelea na kazi na kwa sababu zozote zile ikashindikana kitu ambacho pia hutakiwi kuruhusu kitokee. Mara nyingi sababu zinatokana na uzembe na uvivu wa wahusika na jambo la msingi sana ni kutokuzitambua sababu kiurahisi, ambapo hiyo itapelekea kuwasukuma wahusika kuhakikisha wanafikia viwango kwa kujua kwamba hakuna sababu yoyote watakayoleta itakayokubalika.

INAPASWA IJULIKANE WAZI MWANZONI KWAMBA KAZI ILIYOFANYIKA CHINI YA VIWANGO VILIVYOWEKWA HAITAKUBALIKA

Kazi nyingi za ujenzi zinafanyika chini ya viwango sio kwa sababu ya uwezo mdogo wa wanaofanya peke yake bali mara nyingi kwa sababu ya kuruhusu visingizio ambavyo vinatokana na uvivu, uzembe au tamaa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *