GHARAMA ZA RAMANI YA GHOROFA ZIKO MARA MBILI

Nyumba nyingi zaidi zilizokuwa zinajengwa siku za nyuma ni nyumba za kawaida za kuishi zisizo za ghorofa kwa sababu aidha ya kipato au mazoea. Lakini miaka ya hivi karibuni nyumba za ghorofa zinazojengwa nazo zimekuwa nyingi sana na watu wengi sana siku hizi wanafikia maamuzi ya kuamua kujenga ghorofa kwa sababu mbalimbali. Ni kweli nyumba ya ghorofa japo ina gharama zaidi lakini ni nzuri zaidi hasa kwa mtu mwenye uhitaji wa nafasi kubwa lakini eneo lake la ujenzi ni dogo pamoja na mvuto wa kimuonekano wa jengo.

NYUMBA YA KAWAIDA ISIYO YA GHOROFA INA MFUMO RAHISI WA MIHIMILI

Kitu ambacho watu wengi wamekuwa hawaelewi ni utofauti wa gharama kati ya nyumba ya ghorofa na nyumba ya kawaida. Nyumba ya ghorofa kutokana na changamoto ya kazi husika, umakini unaohitajika katika kupangilia nafasi za vyumba ndani ya jengo pamoja na thamani ya mradi kwa ujumla gharama yake hufikia angalau mara mbili ya gharama za nyumba isiyo ya ghorofa. Hata hivyo kwa nchi yetu nyumba ya kawaida inahusisha gharama moja tu ya michoro ya usanifu peke yake, lakini nyumba ya ghorofa popote pale duniani kwa ajili ya uimara kuna michoro mara mbili. Kwanza kuna hiyo michoro ya usanifu ambayo ndio sawa nay a nyumba ya kawaida halafu pia kuna michoro mingine ya uhandisi mihimili ambayo ni michoro ya mpangilio wa nondo kuanzia ukubwa wake mpaka umbali kati ya nondo moja na nyingine pamoja na vipengele vingine vya mihimili ndani ya jengo lenyewe. Kwa maana hiyo ramani ya nyumba ya ghorofa kwa michoro yote inaweza kufikia mara tatu ya ramani ya nyumba ya kawaida.

NYUMBA YA GHOROFA INA MFUMO TATA WA MIHIMILI

Hata hivyo gharama hizo ni sehemu ndogo sana ya gharama za ujenzi kwa ujumla ambapo mara hazifikii hata asilimia 1% ya gharama zote za ujenzi wa jengo husika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *