GHARAMA ZA “FINISHING” YA NYUMBA

Tulishajadili huko nyuma namna rahisi na haraka ya kuweza kujua wastani wa gharama za ujenzi wa jengo lolote kwa ujumla, kwamba unachukua gharama ya kuja mita moja ya mraba ya jengo husika kisha unaizidisha na idadi ya mita za mraba za jengo unalotaka kujenga na hapo utapata jumla yake ambayo ndio itakuwa wastani wa gharama kwa ujumla. Njia ya kupiga mahesabu ya hivyo inakupa jumla kuu ambayo itakusaidia kujua kwamba mradi huo unaweza kukugharimu wastani wa kiasi gani cha pesa lakini sasa ikiwa unahitaji mchanganuo na orodha ya vifaa vyote na mgawanyiko wa kazi za kiufundi zitakavyokwenda na kugharimu hapo ndio unahitaji mtaalamu wa ukadiriaji majenzi akufanyie kazi nzima ya makadirio kitaalamu.

KUPATA GHARAMA SAHIHI ZA UJENZI UNATAKIWA KUWA NA MICHORO YA HUSIKA NA KUTAFUTA MTAALAMU WA UKADIRIAJI MAJENZI

Tukija sasa kwenye suala la “finishing” ya nyumba ambayo kikawaida huwa na mambo mengi madogo madogo na gharama zake hutegemea na idadi ya vipengele vinavyohitaji kuboreshwa kwa viwango vilivyopangwa pamoja na utata wa vipengele husika kadiri ya umaridadi wake. Lakini kwa makadirio ya haraka ya wastani ni kwamba gharama ya jumla ya “finishing” ya jengo ni nusu ya gharama ya ujenzi wote kwa ujumla. Yaani wastani wa gharama ya “finishing” ni sawa na kuchukua wastani wa gharama ya jengo kuanzia msingi mpaka kupaua, ambapo “finishing” inatumia gharama sawa na gharama ya jengo kuanzia msingi mpaka kupaua. Hii ni kumaanisha wastani wa gharama ya jengo kuanzia msingi mpaka inajumuisha msingi, kuta na kupaua, kisha finishing inaanzia kwenye kupiga ripu/plasta, milango na madirisha kuendelea mpaka kumaliza na kuhamia.

GHARAMA ZA MAKADIRIO HUTOFAUTIANA KIASI NA GHARAMA HALISI KUTEGEMEANA NA SABABU MBALIMBALI

Hata hivyo huo ni wastani wa gharama kwa ujumla kwa makadirio lakini gharama za “finishing” huweza kuongezeka kutakana na utata wa vipengele vyenyewe vya “finishing” ambavyo mara nyingi unatokana na umaridadi wake.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *