KURAHISISHA KUPATA KIBALI CHA UJENZI FIKA HALMASHAURI YA JIJI, MANISPAA AU MJI KABLA YA KUANZA KUTENGENEZA MICHORO.

Katika kufuatilia kibali cha ujenzi ni zoezi ambalo mara nyingi hukutana na changamoto mbalimbali kama vile michoro kutokidhi vigezo vinavyohitajika ili kupewa kibali lakini changamoto kubwa kuliko zote ni kwenye suala la matumizi ya ardhi. Changamoto za mchoro kutokidhi vigezo ni changamoto inayotatuliwa kwa michoro kufanyiwa marekebisho na wataalamu waliofanya michoro hiyo kuendana na vigezo na masharti yaliyowekwa na halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika, zoezi ambalo huwa ni rahisi na halihusishi mchakato wowote mkubwa kuendelea na mchakato wa kupata kibali cha ujenzi. Lakini changamoto ya matumizi ya ardhi ambayo suluhisho lake ni kufanya mabadiliko ya kimatumizi huwa ni zoezi linalohusisha mchakato mkubwa, kuchukua muda na gharama na bado kuna uwezekano wa ombi la kubadili matumizi likakataliwa pia.

MATUMIZI YA ARDHI HUWEZA NA VIPENGELE VINGI ZAIDI KUTOKA KWENYE MATUMIZI YALIYOAINISHWA KWENYE HATI

Hivyo ili kupunguza usumbufu unaojitokeza mara nyingi katika kufuatilia kibali cha ujenzi ni vyema kufika kwanza halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika kwa kuanzia katika idara ya mipango miji ukiwa na hati yako ya kiwanja kujua kwanza kama unachotoka kufanya kinaendana na matumizi husika. Hata ikiwa una uhakika kwamba matumizi ya hati yako yanaendana na unachotaka kufanya ni vyema kwenda kuhakiki kwenye halmashauri ya manispaa husika kwani mara nyingi licha ya kwamba hati imeainisha matumizi kwa uwazi kabisa lakini mipango miji bado wana vipengele vingi sana katika kila matumizi na kwa kuwa hufahamu kipengele kilichowekwa kwenye hati yako bado utakuta mradi unaotaka kufanya unatofauti kidogo na kipengele kilichoanishwa katika matumzi hayo hayo. Kwa mfano unaweza kuona hati imeandikwa ni kwa ajili ya makazi au makazi biashara kisha mbele wakaweka kipengele “c”, ambapo utakuta hicho kipengele “c” kinaashiria kwamba nyumba hiyo ya makazi inatakiwa iambatane na duka kwa nje katika huo mtaa na wewe unapotaka kuweka makazi pekee bila duka inakuwa ni matumizi tofauti na hivyo umekosa vigezo vya kupewa kibali. Changamoto ndogo ndogo za aina hii ni nyingi ndio maana nasema ni vyema kwenda kuanzia halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika kabla ya kuanza kutengeneza michoro ya ramani.

UKIANZIA KWENYE HALMASHAURI YA JIJI, MANISPAA AU MJI HUSIKA ITAKURAHISHIA KAZI NA KUKUEPUSHIA USUMBUFU

Unapokwenda halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika kabla ya kuanza kutengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya mradi wako wa ujenzi ni vyema ukapita kwenye idara zote ambazo michoro hiyo itapita ili kupata taarifa za kutosha na kufanya maandilizi sahihi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *