BAADA YA KIKAO CHA MADIWANI KUONDOLEWA VIBALI VYA UJENZI VINACHUKUA MUDA MFUPI SANA.

Vibali vya ujenzi ni kati ya vitu vilivyokuwa na urasimu mkubwa ambavyo vilikuwa vinachelewesha sana miradi ya ujenzi kufanyika na sekta nzima ya ujenzi imekuwa wahanga wakubwa wa jambo hili. Hata hivyo licha ya kwamba nyaraka za kufuatilia vibali vya ujenzi zinapitia kwenye idara nyingi sana za kwenye halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika lakini changamoto kubwa ilikuwa kwenye kusubiri kikao cha madiwani ambacho kwa baadhi ya halmashauri kilikuwa kinakaliwa mara moja kila baada ya miezi mitatu. Japo wakati mwingine pia idara nyingine za halmashauri kama vile mipango miji, mazingira, afya, ujenzi n.k., zilikuwa zinachelewesha kupitisha nyaraka husika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali lakini ilikuwa ukifanyika ufuatilia thabiti jalada la mzunguko liliweza kutumia muda mfupi hata wakati mwingine wa chini ya wiki moja kumalizika lakini baada ya hapo ililazimu usubiri tarehe ya siku ya kikao cha madiwani ili mradi husika kupitishwa na kupewa kibali.

MIKUTANO YA MADIWANI INAKALIWA KWA NADRA SANA HIVYO ILIKUWA INACHELEWESHA KUPATIKANA KWA VIBALI VYA UJENZI

Jambo hili lilikuwa linaleta usumbufu na limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu kwamba kikao hiki cha madiwani hakina umuhimu katika kupitisha vibali vya ujenzi kwani hakuna chochote cha ziada ambacho madiwani wanaongeza, na kama ikiwa sababu ni migogoro ya ardhi kuna barua maalumu ambayo husainiwa na Mwenyekiti ya serikali ya kijiji ambayo huonyesha kwamba ardhi husika iko sawa na haina mgogoro wowote, lakini hata kama hilo halitoshi basi diwani angeweza kufuatwa ofisini kwake kupitisha badala ya kusubiri wanye kukutana kwa pamoja ambapo inachukua muda mrefu sana. Lakini baada ya serikali kutoa agizo kwamba madiwani waondolewe kwenye mchakato wa kupitisha vibali vya ujenzi kwa sababu wanaongeza urasimu usio wa lazima na kwamba idara za halmashauri zinazohusika na vibali vya ujenzi ndio zikae zenyewe na vikao viwe vinakaa kila baada ya wiki mbili imesaidia sana kupunguza ule usumbufu wa mwanzoni. Hata hivyo changamoto nyingine ndani ya idara za halmashauri husika bado zipo lakini ni jukumu la mkurugenzi na wafanyakazi wengine ndani ya halmashauri husika kuendelea kuongeza ufanisi na ubunifu kupunguza changamoto hizi zinazochelewesha vibali vya ujenzi bila kuwa na ulazima huo. Hata hivyo pia idara nzima za halmashauri pamoja kwa ushirikiano na wizara ya ardhi wanaweza kuongeza ushirikiano na ubunifu zaidi katika kuongeza ufanisi wa kazi ili kurahisishia watu mchakato mzima wa kupata vibali vya ujenzi katika kesi ya changamoto sugu ya matumizi ya ardhi.

KWA SASA VIBALI VYA UJENZI VIKISHAPITISHWA NA KIKAO CHA IDARA HUSIKA ZA HALMASHAURI VINASAINIWA NA MKURUGENZI NA KUTOLEWA

Changamoto ya kucheleweshwa kwa vibali vya ujenzi imekuwa ikiwaathiri sana watu kwa sababu ucheleweshwaji wa miradi ya ujenzi mara nyingi umekuwa ukiambatana na hasara mbalimbali za muda na fedha na wakati mwingine hata kuchangia mradi kushindwa kukamilika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *