KUTUMIA GHARAMA KUBWA PEKEE HAITOSHI, UJENZI BORA UNAHITAJI UTAALAMU SAHIHI.
Imekuwa ni jambo la kusikitisha sana mtu unapokutana na majengo mbalimbali ya makazi, biashara, taasisi mbalimbali, ofisi, viwanda n.k., na kukutana na majengo makubwa ambayo yamegharimu fedha nyingi sana kujengwa lakini yakiwa na ramani za viwango duni sana. Hili linasikitisha sana kwa sababu unaona wazi kwamba fedha iliyotumika kujenga ni kubwa sana na ilihitajika kutolewa pesa kidogo sana ukilinganisha na iliyotumika kujenga kuweza kufanya kazi ya kitaalamu ya jengo bora sana kwa gharama ile ile ya ujenzi iliyotumika lakini kushindwa kufanya maamuzi sahihi hapo kumepelekea kuwa na jengo lenye mwonekano wa hovyo ambao utaendelea kuwa hivyo miaka mingi sana mbele.
Suala la ubora wa kisanifu ni jambo ambalo bado limekuwa halipewa uzito unaostahili licha ya kwamba madhara yake ni makubwa sana mara baada ya kujenga. Changamoto nyingine ni kwamba jengo likishajengwa gharama iliyotumika haiwezi kurudi na ikiwa litahitajika kubomolewa ili kurekebishwa au kufanyiwa ukarabati tayari huo ni upande wa hasara, na hata hivyo bado tatizo husika linaweza lisitatuliwa kiwango kinachohitajika kwa sababu madhara yake kiufundi ni makubwa sana. Ni wakati sasa watu kuongeza uzito zaidi kwenye huduma bora za kitaalamu kabla ya kuanza mradi wa ujenzi kwani hapo ndipo akili inapotumika siku zote, na eneo ambalo akili inatumika ndio eneo lenye uimara siku zote na halijawahi kumwangusha mtu ambaye ametuliza akili yake na kuwekeza hapo kwa umakini. Uzuri ni kwamba kiasi cha fedha mtu unachowekeza kwenye huduma bora za kitaalamu na faida unazopata ni tofauti sana, kwa sababu ni eneo litakalokulipa vizuri sana kuanzia kisaikolojia, kiuchumi, ufahari, uelewa na hata kuepuka majuto na hasara na mwisho wa siku utajiona ni mshindi zaidi.
Faida za kuwekeza kwenye utaalamu bora na sahihi utakuja kuziona mwishoni baada ya ujenzi kwa sababu utakuwa umejikuta ukilazimika kuchanganya malengo yako na taaluma itakayohakikisha yanakaa katika usahihi na uhalisia na kukuletea matokea utakayoyafurahia.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Asante sana kwa kutupatia TAHADHARI juu ya ujenzi wa nyumba bila kutumia Utaalamu.
Rafiki yako,
Aliko Musa