WEKA MPANGILIO SAHIHI WA KIMATUMIZI KATIKA KIWANJA CHAKO KADIRI YA UTAMADUNI WAKO NA MAHITAJI YAKO.

Mpangilio wa kimatumizi ni eneo muhimu sana la kulifanyia kazi kwa ukaribu, umakini na uangalifu pale unapokuwa unatengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya nyumba yako ya kuishi. Mara nyingi watu wamekuwa wakimwachia mtaalamu wa usanifu kuamua namna atapangilia mwenyewe kadiri anavyofikiri inafaa kitaalamu bila kujua kwamba anayeenda kutumia eneo hilo sio mtaalamu bali ni yeye mwenyewe. Mwisho wa siku anakuja kujikuta hafurahii kilichofanyika kwa sababu hakuangalia utamaduni wake na mtindo wake wa maisha katika kufanya mipangilio.

UTAMADUNI WAKO UTAAMUA MPANGILIO SAHIHI WA ENEO LAKO LA MAKAZI

Kazi hii ya kufanya mipangilio ya kimatumizi katika eneo la makazi yako ni muhimu sana kushiriki moja kwa moja kwa sababu kwa mfano labda wewe unajijua ni mtu mwenye marafiki wengi na ambaye mara kwa mara, pengine hata kila mwezi huwa unafanya sherehe na kutembelea na marafiki zako wengi aambao wote wana usafiri binafsi na eneo ulilopo hakuna maegesho ya magari zaidi ya ndani ya uzio. Ni wazi kwamba hapo unahitaji kuweka idadi ya maegesho ya gari ya idadi unaiyojua wewe mwenyewe ambayo mtaalamu hawezi kujua lakini mtaaalamu kwa kuona kipaumbele chako hicho atajitajidi kupangilia matumizi ya eneo hilo kwa namna ambayo itatoa kipaumbele kwa maegesho ya magari kwa idadi hiyo. Inawezekana ikawa labda wewe unapenda kukaa kimya ndani na kujisomea, kufanya maombi au kufanya tahajudi hivyo mpangilio wa eneo ambalo chumba chako na ofisi yako vitakaa na matumizi yatakayokuwepo upande huo wa kiwanja yawe ambayo hayaleti usumbufu kwako kwa namna unavyohitaji iwe. Hii itakufanya ujisikie huru zaidi na kupenda nyumbani kwako na eneo lako kuliko kumwacha mtu akuamulie halafu mwisho wa siku ikiwa havitaendana na tabia na utamaduni wako vitakupunguzia uhuru na furaha ya maisha yako.

NI MUHIMU SANA KUFIKIRIA KWANZA AINA YAKO YA MAISHA ILI KUWEZA KUYAHUSIANISHA NA NAMNA UNAFANYA MPANGILIO WA ENEO LAKO LA MAKAZI

Kimsingi mpangilio wa kisanifu wa eneo lako unafanya na wewe mwenyewe lakini kwa msaada wa mwongozo wa kitaalamu kutoka kwa mtaalamu husika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

1 reply
 1. UWEKEZAJI MAJENGO
  UWEKEZAJI MAJENGO says:

  Asante kwa maarifa mazuri sana.

  Wengi tunatoa maelezo machache mno kwa wasanifu majengo.

  Kiasi kwamba inakuwa vigumu Kuandaa jengo ambalo linaendana na utamaduni wa maisha ya mwenye nyumba.

  Asante sana kwa kunifundisha hili rafiki yangu Architect Sebastian Moshi.

  Rafiki yako,

  Aliko Musa.

  Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *