MAEGESHO YA WAZI YA VIVULI VYA MAGARI KATIKA ENEO LA MAKAZI (CAR PARK SHADE).

Katika mpangilio wa eneo lake la makazi nyumbani moja kati vitu muhimu sana vya kuzingatia ni maegesho ya magari. Japo hata hivyo kuna utamaduni wa miaka ya nyumba kidogo ambao hata mpaka sasa bado unawavutia watu wengi wa kuweka maegesho ya magari ndani ya nyumba.

Utamaduni wa kuweka maegesho ya magari ndani ya nyumba sio utamaduni mbaya na wakati mwingine ndio mbadala pekee kutokana na ukubwa wa kiwanja au mpangilio wa eneo husika la makazi lakini changamoto yake kubwa ni gharama kubwa ukilinganisha na maegesho ya kivuli cha wazi.

MAEGESHO YA MAGARI YA NDANI YA NYUMBA

Kitaalamu inapendekezwa kwamba ikiwa huna changamoto ya eneo, yaani eneo la kiwanja chako linaanzia angalau ukubwa wa mita za mraba 400 basi ni bora ukachukua mbadala wa kuweka maegesho ya wazi ya vivuli vya magari nyumbani kwako badala ya kuweka maegesho ndani ya jengo.

Hii kwa sehemu kubwa ni kwa sababu ya gharama, kwani maegesho ya ndani ya nyumba/jengo yanachukua sehemu kubwa ya jengo na inaongeza sana gharama za jengo kwa mfano gharama inayoongezeka kwa kuweka maegesho ya gari moja ndani ya jengo inafika mara tatu ya gharama ya kujenga vivuli vya maegesho ya wazi ya magari matatu.

MAEGESHO YA WAZI YA KIVULI CHA GARI (CAR SHADE)

Hii ni kumaanisha kwamba gharama inayoongezeka kwenye ujenzi wa jengo husika kwa kuweka maegesho ya gari moja tu ndani ya jengo ni mara tatu ya gharama ya kuweka maegesho ya wazi ya vivuli vya magari matatu ndani ya jengo, yaani gharama ya maegesho ya gari moja ndani ya jengo unaweza kujenga maegesho ya vivuli vya wazi vya magari tisa.

MAEGESHO YA VIVULI VYA WAZI

Pia gari linapokuwa kwenye maegesho ya vivuli vya wazi nje ya jengo linakuwa huru zaidi kulitumia wakati wowote na mtu yeyote kuliko ambalo limefungiwa ndani ya jengo. Hta hivyo gari kukaa ndani ya jengo linakuwa na usalama mkubwa zaidi hasa dhidi ya watu wa nyumbani na ni eneo ambalo unakuwa umelificha pia ikiwa huhitaji lionekana na wageni waliofika nyumbani kwa dharura.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *