TENGENEZA PARADISO YAKO HAPA DUNIANI.

Watu wengi wanoamini neno la Mungu wanaamini kwamba baada ya maisha ya hapa duniani wataenda kuishi paradiso, sehemu yenye kuvutia sana watakayoishi kwa raha mustarehe baada ya matendo mema na imani kwa Mungu wakiwa hapa duniani. Na kwa hakika hilo ni jambo jema sana.

Paradiso ni eneo lenye uzuri wa asili, lenye kuvutia sana lisilokuwa na mfano na lenye kila kitu ambacho mtu anahitaji ili kufurahisha roho na nafsi yake ambalo ni tulivu na mahsusi kwa ajili ya kupumzika.

Lakini ukweli ukiamua unaweza kutengeneza paradiso yako mwenyewe hapa duniani kwa kadiri ya mipango yako, paradiso yako ambayo itakupa vitu vingi vinavyoweza kufikirika ambavyo viko kwenye paradiso unayoisikia kutoka kwenye vitabu na kuongezea ambavyo ni vya kipekee kwako binafsi.

UNAWEZA KUTENGENEZA PARADISO YAKO HAPA DUNIANI

Unachotakiwa kufanya ni kuorodhesha vitu vyote vya kipekee vinavyokuvutia sana kutoka kwenye unayojua, uliyosikia, uliyoona katika tamthilia na ambayo umekutana nayo yakakufurahisha sana.

Paradiso yako ni makazi yako ambayo yatajumuisha kila kitu kuanzia kuanzia nyumba mpaka mandhari bora kabisa ya asili unayoipenda ambayo imepangiliwa kwa usahihi na kitaalamu sana kuanzia upoingia getini unakuwa umeingia kwenye paradiso kamili mpaka kuzunguka mandhari yote ya nyumba kila kitu katika hadhi ya paradiso kamili.

Wengi wetu hapa duniani tumeshakutana na maeneo ambayo kiuhalisia ni paradiso katika akili zetu, maeneo mengi yakiwa ni ya biashara kama vile hoteli za kitalii au maeneo mengine ya kupumzika na machache mengine yakiwa makazi ya watu walioamua kutengeneza paradiso zao hapa duniani.

Habari njema ni kwamba kutengeneza paradiso yako huhitaji kuwa na pesa nyingi sana, au angalau huhitaji kuwa na pesa nyingi sana kwa wakati mmoja, kikubwa unachohitaji ni mipango sahihi.

PARADIO YAKO ITAKUWA NA VITU VINAVYOKUVUTIA WEWE KIPEKEE

Kwanza kabisa unachohitaji kwa sasa hivi ni kujua kwanza unahitaji paradiso yako ijumuishe nini na nini haswa, ufanye kuorodhesha kila kitu unachohitaji kiwepo ndani ya paradsio yako kisha kutafuta mtaalamu mtakayejadiliana naye juu ya ukubwa wa eneo linaloenea kila kitu kilichopo kwenye paradiso yako.

Baada ya hapo utaanza kwanza kwa kutafuta eneo ambalo linaenea kila kitu kilichopo katika paradiso yako na kisha kurudi kwa mtaalamu ambapo mtaanza sasa kuitengeneza paradiso hiyo katika michoro na kukamilisha kila kitu. Ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya paradiso yako ni mpangilio sahihi wa mandhari yako ikiwa sehemu kubwa ni mazingira asili.

PARADISO NI HALISI KAMA ILIVYO AKILINI MWAKO

Baada ya kukamilisha mpangilio mzima wa paradiso yako kwa namna ambayo itakuwa imekuridhisha kwamba ni hiyo paradiso hasa unayoihitaji ndipo utekelezaji utaanza taratibu kuelekea kukamilisha kila kitu kilichopo kwenye michoro ya paradiso yako.

Utashangaa paradiso yako inaendelea kukamilika taratibu kuelekea kuwa eneo litalokuvutia kuliko eneo lingine lolote ulilowahi kuwepo, lakini hili litakuwa ni nyumbani kwako.

Nikutakie kila la kheri unapoendelea kuifikiria na kuipangilia paradiso yako.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *