VIWANJA VINGI NI VYA MAKAZI PEKEE

Kupata kibali cha ujenzi limekuwa ni suala lenye changamoto kubwa kwa miradi mingi isiyo ya makazi kwa sababu viwanja vingi ni kwa matumizi ya makazi pekee.

Hata hivyo katika kununua viwanja watu wengi japo huwa na mawazo ya kuendeleza maeneo husika kwa miradi ya aina tofauti lakini huwa hawajihangaishi sana kuchunguza matumizi ya eneo hilo.

Baada ya mtu kuwa amemaliza mpaka kazi nzima ya michoro na kwenda kufuatilia kibali cha ujenzi ndio hugundua kwamba matumizi anayoyalenga hayaendani na matumizi yaliyopangwa na mamlaka za mipango mjiji kwa kiwanja husika.

Kwa sababu hiyo hupelekea vibali vya ujenzi kukwama na hii ni kutokana na matumizi yanayopangwa na mamlaka za mipango miji kwa sehemu kubwa ni matumizi ya makazi pekee.

Hili huwa changamoto zaidi kwa sababu hata kwa matumizi ya makazi pekee unaweza kukuta nyumba ya makazi ikaonekana haikidhi vigezo vya matumizi ya kiwanja husika kutegemea na namna ilivyopangiliwa kwamba kama itaonyesha dalili kwamba ni ya biashara hata kama kweli ni makazi bado inaweza kunyimwa kibali cha kuendeleza.

Lakini kwa kuwa watu huwa tunabadilisha mawazo kila siku kutokana na kubadilika kwa mipango, hali ya kiuchumi na fursa mbalimbali zinazojitokeza, sio mara zote mtu atataka kutumia kiwanja husika kwa matumizi yaliyopangwa na wizara, badala yake anaweza kubadili mawazo muda wowote.

Sasa katika kubadilika badilika kwa mipango na malengo yako binafsi, ni vyema unapotaka kujenga eneo lako mkazungumza na mtaalamu kuona namna mnaweza kulipangilia eneo kwa namna ambayo litaendana na matumizi yaliyopangwa bila kuathiri sana kile unachoamua kufanya.

Karibu sana kwa huduma mbalimbali za kitaalamu

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *