GHARAMA SAHIHI YA UJENZI INAPATIKANA BAADA YA MICHORO KUKAMILIKA.

Gharama za ujenzi wa mradi ndio kitu cha kwanza ambacho karibu kila mteja amekuwa akitaka kukifahamu mara baada ya kukutana na mtaalamu kujadili mradi husika, na hilo ni sahihi kabisa kwa sababu fedha ndio inayoamua kuhusu utekelezaji wa mradi husika.

Hata hivyo licha ya kwamba kuna uwezekano wa kufanya makadirio ya gharama za mradi wa jengo husika lakini hilo litakuja baada ya michoro ya ramani za jengo husika kukamilika, bila kuwa na michoro ya ramani za jengo husika unakuwa bado huna kitu ambacho unaweza kukifanya makadirio.

Michoro ya ramani yenyewe hupatikana baada ya kufahamu taarifa zote za eneo la ujenzi kisha mahitaji ya mteja kufafanuliwa kwa usahihi na michoro ya ramani kutengenezwa kwa kadiri ya mahitaji na mapendekezo ya mtaji kwa kuzingatia kanuni za kitaalamu ndipo ukubwa halisi kupatikana.

Baada ya kupata ukubwa halisi kutoka kwenye kazi ya usanifu wa michoro ya ramani za ujenzi uliozingatia uhalisia wa kile hasa kinachotakiwa katika viwango sahihi ndipo makadirio ya gharama za ujenzi yanaweza kupatikana kutokea kwenye michoro hiyo.

Hii ni tofauti na dhana iliyozoeleka kwamba mtu anaweza kukwambia umwambie gharama za kujenga nyumba ya kuishi kwa mfano ya vyumba vitatu au vine na ukamtajia kwa makadirio kwa kukisia ukubwa halisi unaoujua mwenyewe, lakini baada ya michoro kukamilika na ikawa na ukubwa wa tofauti au eneo jengo linapojengwa kukawa na changamoto za tofauti gharama hiyo lazima itabadilika.

Hivyo ni muhimu kujua kwamba gharama halisi na ambazo zitaendana na uhalisia wa mradi husika zitapatikana kwa uhakika baada ya michoro kukamilika.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *