WATU WENGI WALIOJENGA KWA RAMANI ZA KWENYE MITANDAO BILA KUHUSISHA MTAALAMU WAMEISHIA KWENYE MAJUTO.

Kuna watu wanaamini kwamba ramani za kujenga nyumba zinapatikana kwenye mitandao, wakati mwingine ni ushauri kutoka kwa marafiki au watu wa karibu kwamba kama unataka kujenga nyumba unaweza kuchukua ramani kwenye mitandao.

Ukweli ni kwamba kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 95% kwamba ramani unayoitoa kwenye mitadao haikufai, hata kama umeinunua kwa pesa kama aliyekuuzia huwezi kuwasiliana naye mkaijadili kama kama inakufaa au inahitaji mabadiliko basi hiyo sio sahihi kwako.

Ni muhimu kufahamu kwamba kila mtu ana mahitaji yake ya kipekee na mambo anayoyapendelea binafsi lakini licha ya hivyo kila mtu ana vipaumbele vyake ambavyo ni tofauti kabisa na vipaumbele vya mtu mwingine, unapochukua ramani ambayo imefanywa kwa ajili ya mwingine ni vigumu kukufaa.

Kutokea kwenye uzoefu wangu binafsi ni nadra sana tena sana ukakuta vipaumbele vya watu wawili tofauti vikafanana kwa asilimia 100%, mara nyingi utakuta kuna utofauti lakini hata ikitokea vipaumbele vikakaribia kufanana au kufanana kabisa utakuta utofauti unakuja kwenye ukubwa wa kiwanja au kwenye utofauti wa kipato au kwenye masharti ya mamlaka za sehemu husika au hadhi ya kiwanja n.k.,

Hivyo hata sisi wenyewe japo baadhi ya watu hufikiri tunapata ramani mitandaoni lakini huwa ni vigumu sana mtu kuingia mtandaoni akapata kweli ramani ya kile anachokitaka, kiasi kwamba wataalamu hata huwa hawajihangaishi na ramani za mitandaoni isipokuwa tu kwa ajili ya kujifunza.

Kwa hiyo kwa watu ambao hujaribu kulazimisha kuchukua ramani ya ujenzi mtandaoni na kwenda kuijenga baada ya muda hugundua amefanya kosa na kwamba kile alichokuwa anafikiria ni tofauti na uhalisia na tayari yuko upande wa hasara iwe ataendelea na kazi hiyo au ataamua kuachana nayo. Hivyo mtu kuishia kwenye majuto na maumivu kwani kuendelea haifai na kubadilisha ni hasara kubwa ya fedha.

Hivyo ni muhimu sana kufahamu kwamba ramani za kuchukua mitandaoni zina usumbufu mkubwa na mara nyingi itakuingiza kwenye aidha hasara au majuto au vyote kwa pamoja.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *