“USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA”, VIKAO NI MUHIMU SANA KATIKA MRADI WA UJENZI.

Kuna huu msemo maarufu wa kiswahili unaosema “usipoziba ufa, utajenga ukuta” ni msemo ambao una umuhimu mkubwa kwenye baadhi ya maeneo na hapa tunaona ukiingia kwenye hili eneo la ujenzi. Katika mradi wowote wa ujenzi vikao vya kuhusu maendeleo ya mradi husika ni muhimu sana katika kuepuka kuingia kwenye changamoto kubwa au hasara kubwa.

Tunafahamu kwamba makosa katika miradi ya ujenzi ni jambo la kawaida na la kila siku lakini mbali na makosa pia kuna mabadiliko ambayo huweza kutokea kwa sababu mbalimbali, mengine ni ya lazima na mengine sio ya lazima lakini yenye umuhimu mkubwa ambapo haya yote huwa sahihi zaidi kujadiliwa katika vikao ili kuweza kuingizwa kwenye utekelezaji au mabadiliko husika kuchukua nafasi.

Kuwepo kwa vikao vya mara kwa mara kutasaidia katika kufikia maamuzi sahihi na yenye tija kwa pande zote zinazohusika na kuepusha mivutano, hasara na kutengenezwa kwa changamoto ambayo sio rahisi tena kurekebishika kwa sababu ya umbali ambao mradi umefikia.

Hivyo ni muhimu sana katika mradi wowote wa ujenzi ili kufikia matokeo ya viwango bora na yaliyokidhi mahitaji ya kila upande unaohusika kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa kila hatua kujadili mwenendo wa mradi sambamba na changamoto zinazoambatana nao na kuzitatua ili mtu uzibe nyufa mapema kabla hujachelewa na kujikuta unajenga ukuta.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *