BAJETI YA UJENZI ULIYOPANGA HAITATOSHA

Kati ya vitu ambavyo sisi binadamu tumekuwa tunapenda ni kitu kinaitwa uhakika kinachoambatana na usahihi wa vitu. Hata mawazo yetu watu wengi tukifikiria huwa tunafikiria katika uhakika na usahihi lakini kwa bahati mbaya dunia sivyo ilivyo, vitu vingi duniani huwa havina usahihi wala uhakika na ni mara chache sana kukuta kitu chochote kile chenye usahihi na uhakika.

Kwenye ujenzi napo mambo hayako tofauti sana na asili hii. Mara nyingi utakuta mtu anakwambia nataka uniambie gharama ya kujenga nyumba ya kuishi ya vyumba vitatu, unamwambia inabidi tufahamu kwanza ukubwa wake lakini kwa sababu haupo tufanya kudhani ukubwa fulani kisha unamwambia ukubwa huo na makisio ya gharama.

Lakini yeye katika akili yake anataka kujua kiasi haswa kinachotosha bila kuongezeka au kupungua, unajaribu kupungua gharama hiyo itategemea na vitu vingine vingi sana kwa sababu gharama za malighafi zinatofautiana sana kulingana na ubora, ukubwa na vitu vingine lakini pia gharama za ufundi ziko tofauti sana pia kutegemeana na viwango mbalimbali vya ubora wa ufundi wenyewe.

Basi kwa vipengele vyote mnaamua kudhania(ku-assume) ili aweze kupata gharama kamili anayohitaji, unamwambia gharama lakini unamjulisha pia kwamba huenda kukawepo dharura mbalimbali ambazo nazo huenda zikaongeza pia gharama hizo, na hapo mnaamua kuweka na hizo dharura ili mpate gharama kamili ijulikane kabisa kwa usahihi.

Lakini kwa baadhi ya miradi kama kuna maeneo hamkuyatafiti vizuri bado utakuta bajeti inaenda tena zaidi ya ile mliyokadiria na hapo ndipo mteja anapofikiri kwamba hukumwambia ukweli. Kiuhalisia ukweli ni kwamba ni mara chache sana bajeti inayopangwa katika mradi wa ujenzi kutosha kabisa bila gharama zozote kuongezeka, mara nyingi bajeti huwa hivyo kwa miradi yote. Hata katika miradi mikubwa ya serikali ambayo kila kitu na kila dharura hujumuishwa bado utakuta miradi mingi inakwenda nje ya bajeti.

Nafikiri hata wewe kwenye mambo yako mengi ambayo huwa unapanga yanayohusu fedha huwa mwisho wa siku unajikuta bajeti uliyoiweka inapelea na kama haukuwa makini unaweza kukuta gharama zinakuwa kubwa sana mbali kabisa na vile ulivyofikiri. Hii mara nyingi ni sheria ya asili ambayo huwa inatokea karibu kwenye kila kitu.

Hivyo ni muhimu sana kujiandaa kisaikolojia kwamba bajeti hiyo inaweza isitoshe licha ya kupanga mikakati kwa umakini mkubwa. Lakini hata hivyo endapo utajitahidi kuweka umakini mkubwa na kufanya utafiti wa kina huku usimamizi wa mradi ukawa katika umakini mkubwa sana kuendana na muda unaopangwa basi hata kama kutakuwa na mapungufu yatakiwa ni kidogo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *