KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI PUNGUZA NYUMBA.
Suala la kupunguza gharama za ujenzi ni suala ambalo hufikiriwa na kila mtu anayetaka kujenga lakini changamoto ni kwamba wengi aidha hawajui maeneo ya kuzingatia katika kufanya hivyo au huwa wanaamini kwamba kuna miujiza inaweza kufanyika katika kupunguza gharama za ujenzi.
Kama vitu vinavyofanya gharama iwe kubwa ni vitu unavyovihitaji sana na haupo tayari kuvikosa na pia una uwezo wa kumudu gharama yake hata kama ni kwa muda fulani basi hupaswi kuviondoa bali unapaswa kupambana mpaka uhakikishe vimeweza kukamilika.
Nafikiri jambo la kwanza muhimu kabisa kabla ya vyote ni kufahamu gharama zenyewe za ujenzi ni kiasi gani na kwa nini ni kiasi hicho kwa kujua ni maeneo gani yanafanya gharama iwe kiasi hicho na kisha kuangalia kama ni vitu unavyoweza kufanyia kazi na kama ni gharama unayoweza kumudu au la.
Lakini kwenye suala la kupunguza gharama ujenzi hakuna miujiza bali kitu cha muhimu na kucheza na namba hivyo eneo la kuweka umakini na umuhimu mkubwa katika kupunguza ukubwa wa jengo na wingi wa vitu visivyokuwa na maana kwako.
Kwa sababu kadiri jengo linavyokuwa kubwa na kuwa na vitu vingi ndivyo kadiri linavyokuwa na gharama kubwa katika kulijenga na hakuna njia ya mkato ya kupunguza sana gharama zaidi ya kupunguza ukubwa wa jengo pamoja na wingi wa mahitaji yako ndani ya jengo hilo.
Maeneo mengine kupunguza gharama ukiondoa kupunguza ukubwa wa jengo ni maeneo ambayo gharama zitapungua kwa kiasi kidogo sana au kama utataka kupunguza kwa kiasi kikubwa basi hata uimara na ubora wa jengo lenyewe utakuta unapungua sana kitu ambacho pengine hutapenda kuona kinatokea.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Asante sana kwa somo zuri.