KWENYE UJENZI EPUKA HISIA, FUATA USHAURI WA SAHIHI.

Ninaweza kusema kwamba kati ya vitu ambavyo vimewagharimu sana watu kwa ujumla kwenye kufanya maamuzi hususan masuala ya ujenzi ni kwenye kutanguliza hisia mbele sehemu ya kufuata ushauri sahihi. Sio kwamba watu wanakuwa hawajapata tahadhari kwamba yanayokwenda kufanyika yanaweza kusababisha uharibifu au kazi ya viwango duni, bali ni kwamba wanakuwa bado ni wadhaifu sana kukabiliana na hisia zao na kupingana nazo kiasi kwamba inakuwa rahisi kuangukia kwenye maamuzi mabovu.

Hisia ni zile njia rahisi au zilizozoeleka au ambazo zinavutia ambazo mtu huzifuata au hujikuta ameshazifuata wakati anafanya maamuzi muhimu katika jambo lolote bila kuzingatia usahihi wake au umuhimu wake. Kwa mfano mtu anapoambiwa beo ya vitu viwili halafu anakimbilia kwenye ile bei iliyo rahisi bila kujali ubora wa kitu husika au mtu anapopewa majukumu mawili halafu anakimbilia kwenye lile jukumu rahisi au lisilo na changamoto kubwa bila kufikiria ubora wa matokeo ya kile ambacho jukuu husika litazalisha. Huku ndio kutawaliwa na hisia zaidi bila kujali matokeo.

Changamoto kubwa zaidi ni kwamba watu wengi huwa hata hawajui wakati ambapo wanatumbukia kwenye maamuzi mabovu kwa kufuata hisia kwani wakati huo hisia zinakuwa zimewatawala kiasi kwamba ni mpaka pale mambo yanapokuwa yameharibika na hisia zimeondoka ndipo wanakumbuka kwamba walifanya maamuzi yasio sahihi na kutokana na maumivu yaliyoletwa na hasara au uharibifu mwingine uliotokea ndipo wanapoona kwamba walipaswa kufuata njia sahihi.

Hivyo jambo la msingi la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba muda wote ambao unataka kufanya maamuzi muhimu katika hatua yoyote ya ujenzi kuanzia kununua kiwanja, kutengeneza michoro ya ramani, kusajili mradi, kutoa kazi ya kujenga kwa usahihi pamoja na ushauri mwingine wowote utakaopupata kutoka kwa wataalamu au wabobezi unazingatia sana usahihi wa kitu na sio urahisi wake.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *