KUCHORA RAMANI YA JENGO AMBALO LIPO.

Kwa sababu mbalimbali kuna wateja ambao huhitaji ramani ya jengo ambalo lipo site au kuhitaji jengo hilo kurudia kuchorwa na kufanya mabadiliko kidogo. Kwa bahati mbaya kwa kuwa jengo lenyewe lipo basi watu hufikiri kwamba kulichora ni rahisi kwa sababu tayari lipo. Lakini kiuhalisia jengo ambalo lipo ni kazi ngumu zaidi kulichora kuliko jengo ambalo halipo kabisa kwa sababu kwa jengo ambalo lipo hapa unakuwa kazi mara mbili zaidi ya eneo ambalo hakuna hakuna jengo.

Hili limekuwa likiwashangaza watu lakini huo ndio uhalisia kwa sababu unahitaji kufanyia kazi mara mbili na hivyo kazi kuwa kubwa zaidi hata ya mtu aliyepewa kuchora jengo jipya kwa sababu anafanya kazi mara moja peke yake.

Kazi hii ya kuchora jengo ambalo tayari lipo ili kupata ramani za kutumia kwa usahihi maeneo mengine kwa kuanza kitaalamu huwa inaitwa “documentation” ambayo mara nyingi ndio inaonyesha vipimo vyote ambavyo ndio mtaalamu anavitumia  kuchora upya ramani ya nyumba au kuongezea yale ambayo ni muhimu ambayo yalikosekana bado kunakuwa hakuna shida sana.

Karibu sana,

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *