MATOKEO YA UJENZI DUNI NI YA TARATIBU NA YA MUDA MREFU SANA.

Kati ya maeneo ambayo ni rahisi kufanya makosa na kudhani kwamba umefaidika kiurahisi na kumalizana na jambo husika basi ni katika eneo la ujenzi. Watu wengi hutafuta urahisi wa gharama za ufundi na vifaa na kuona kwamba wamefanikiwa kupata kwa bei rahisi na kukamilisha ujenzi kwa mafanikio lakini ni baada ya miaka kadhaa mbele ndio mtu huja kugundua kwamba alifanya makosa.

Unapokutana na wataalamu wenye huduma bora lakini ambao wana gharama tofauti na watu wengine wa kawaida wasio na huduma bora huweza kuhisi kwamba wataalamu wanaumiza sana na kwamba wangeweza kufanya kwa urahisi. Lakini baadaye unapokuja kufanya tathmini ya jengo ndipo unagundua kwamba hasara uliokuja kupata baada ya muda mrefu ni kubwa kuliko kiasi cha fedha ulichookoa mwanzo na bado utatakiwa kurudia rudia mara kwa mara.

Hivyo ni muhimu sana kwamba kabla hujafanya maamuzi kwa kufuata hisia za kuangalia urahisi na njia ya mkato ni vyema na muhimu sana kufikiria kwamba matokeo ya huduma viwango vya huduma husika vitakuja kuonekana baada ya muda mrefu mbele. Matokeo mabovu ya haraka sana huweza kuonekana kama kuna makosa makubwa sana na ambayo ni muhimu sana. Lakini kwa uduni wa huduma kawaida utaona changamoto yake baada ya muda mrefu sana.

Ahsante sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *