TAALUMA YA USANIFU MAJENGO

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

– Peter Keating anaenda New York kufanya kazi kwenye kampuni ya Usanifu Majengo ya Guy Francon inayoitwa Francon & Heyer.

– Howard Roark naye anaenda New York kufanya kazi kwenye kampuni ya Henry Cameron.

– Henry Cameron ni Msanifu Majengo mkongwe aliyefanya kazi nyingi sana lakini mwenye udhaifu katika eneo la mawasiliano ya umma (Public relations), hivyo baada ya mtaalamu wake mahiri wa kwenye eneo la mawasiliano ya umma kufariki Henry Cameron alirudi nyuma sana na kufilisika kuwa duni sana huku akiendesha kampuni yake katika mazingira magumu sana.

– Lakini Henry Cameron anaonekana ni mtaalamu mbobezi mwenye uwezo mkubwa na anayeipenda sana kazi yake.

– Henry Cameron anashangaa Howard Roark kwa nini ameacha kwenda kutafuta kazi kwenye makampuni makubwa yanayoweza kumlipa vizuri akaja kuomba kazi kwake. Henry Cameron amemwambia Howard Roark kwamba atamlipa dollar 15 kwa wiki na Howard Roark amekubali. Howard Roark ameweka msimamo kwamba anataka kufanya kazi na Henry Cameron.

– Peter Keating anakutana na draftsman anayeitwa Tim Davis kwenye kampuni ya Francon & Heyer na anagundua huyo ndiye draftman(mchoraji) anayependwa na kukubalika zaidi kwenye kampuni na wanakuwa marafiki.

– Peter Keating anamkumbuka(anam-miss) mpenzi wake aliyempenda sana alipokuwa chuoni Stanton aliyeitwa Catherine Hensiy kisha anamtafuta.

– Peter Keating anafanikiwa kumpata Catherine na wanakutana tena. Wanapata muda wa kuwa pamoja na Catherine anamwambia wazi Peter bila kificho kwamba anampenda sana.

– Peter anamshangaa Catherine na kumwambia sio sahihi kumwambia mtu moja kwa moja kwamba unampenda sana kwa sababu anaweza kukuchukulia poa na kukuacha. Catherine anamwambia yeye haoni sababu ya kwa nini afiche ukweli kwamba anampenda sana na anaamini kwamba yeye Peter hawezi kumwacha kwa sababu amekuwa wazi namna hiyo.

– Catherine anamwambia Peter akutane na mjomba wake ambaye ndiye mlezi wake baada ya mama yake kufariki. Catherine anamwambia Peter kwamba mjomba wake ni mtu mzuri sana na mwelewa. Peter anakubali na kusema hata yeye atafurahi kuonana naye na anaahidi ataonana naye.

– Lakini Peter anapogundua kwamba mjomba wake Catherine ni Ellsworth Toohey anamkatalia. Anasema hawezi kuonana na Ellsworth Toohey kupitia Catherine kwa sababu ana mipango yake mingine ambayo hatataka kukutana huko kuwe kumeunganishwa na Catherine.

– Howard Roark anafanya kazi kwenye ofisi ya Henry Cameron. Henry Cameron anagundua kwamba Howard Roark ana kipaji kikubwa sana na uwezo mkubwa sana kwenye kazi za designing.

– Henry Cameron anarudia tena kumshauri Howard Roark atafute ofisi kubwa itakayomtumia vizuri na kumlipa vizuri. Anamwambia kwamba pale kwake anapoteza muda na hatakua zaidi atarudi nyuma kiuwezo.

– Henry Cameron anamwambia yuko tayari kumwombea kazi kwa Guy Francon na hawezi kukutana japo Guy Francon mwenyewe Henry Cameron alimfukuza kazi kwenye kampuni yake zamani.

– Howard Roark anaonekana kukataa na kutaka kubaki kwenye ofisi ya Henry Cameron.

– Henry Cameron anajaribu kumweleza ukweli wa madhara yatakayompata miaka ya baadaye kama hatabadilika. Henry Cameron anamwambia Howard Roark juu ya fedheha na manyanyaso yatayotokana na umaskini wake ambayo yataathiri mpaka taaluma yake.

– Henry Cameron anamuuliza Howard Roark kama hayo ndio maisha anayatarajia huko mbeleni, lakini Howard Roark anaendelea kubaki na msimamo wake wa kuendelea na kazi katika ofisi ya Henry Cameron.

– Tim Davis anafukuzwa kazi kwenye kampuni ya Francon & Heyer baada ya kuoa na kujikuta ufanisi wake unashuka sana. Anashangaa sana kwa nini amefukuzwa kazi lakini hakuna mtu mwingine anayeshangaa.

– Guy Francon anampenda sana Peter Keating na anaenda naye kwenye maeneo mengi na kwenye matukio mengi muhimu na kumtambulisha. Anajivunia sana kwamba Peter Keating ni mfanyakazi wake na kwamba ana uwezo mkubwa japo Peter Keating mwenyewe anaonekana hajiamini sana.

– Peter Keating anamsaidia Tim Davis kupata kazi sehemu nyingine na anajivunia sana juu ya msaada huo alitoa kwa rafiki yake.

– Strengel naye anaacha kazi kwenye kampuni ya Francon & Heyer na kwenda kufungua ofisi yake baada ya kusaidia na Peter Keating kupata moja kati ya mradi ya kuanzia.

– Strengel alikuwa ndiye mtu anayetegemewa sana kwenye kampuni ya Francon & Heyer na ndio amefanya kazi nyingi na ku-design majengo mengi sana.

– Peter anakuwa ndiye manager mkuu wa utendaji kwenye kampuni ya Francon & Heyer lakini haamini sana kazi zake hivyo anazichukua na kwenda nazo kwa Howard Roark kutaka ushauri wake.

– Howard Roark anaziangalia kazi za Peter na anaona kama ni kazi duni hivyo anajaribu kutengeneza concepts mpya na kumpa Peter ambaye anaenda kuziendeleza na kufanya presentation kwa Guy Francon.

– Peter Keating anajaribu kumshawishi Howard Roark ahamie kwenye kampuni ya Francon & Heyer ili aweze kuwa na kipato kikubwa aondokane na maisha magumu na ya fedheha aliyonayo lakini Howard Roark anaonekana kutokukubaliana na wazo hilo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *